Mkuu wa wilaya ya Kilombero ndugu James Ihunyo, akizungumza na wanakijiji wa mang'ula kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa wilaya ya kilombero Ndg James Ihunyo, jana alifanikiwa kufanya uzinduzi wa chanjo ya mlango wa shingo ya kizazi kwa watoto wenye umri wa miaka 14.Kuzinduliwa kwa chanjo hiyo kunafungua mlango kwa watoto wote wenye umri huo kupata chanjo hiyo kwenye wilaya ya Kilombero.
Akitoa rai yake Mhe. Ihunyo alisisitiza kuwa wananchi wa wilaya ya kilombero wanapaswa kuwa makini sana na maneno yanayosemwa mtaani kuwa dawa hizi zina madhara makubwa mbeleni kuwa watu hao ni waongo na hawawatakii mema, dawa hizi hazina madhara yoyote yale kiafya zaidi ya kujikinga na ugonjwa huu ambao ni hatari sana kwa wanawake na watoto, hivyo alishauri kuwa wananchi waupokee mradi huu kwa mikono miwili ili waweze kujikinga na ugonjwa huu.
Awali akitoa ripoti ya chanjo hiyo, mratibu wa Afya wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, bi Niindaeli Malugu alisema kuwa ugonjwa huu umekuwa ni tishio kubwa sana hususan kwa mabinti wadogo kuanzia miaka 14 kutokana na ukweli kwamba mabinti wengi huanza mapenzi wakiwa na umri mdogo sana, hivyo kupelekea kuathirika kwa kiwango kikubwa sana kwa wasichana hao.
Aidha akielekeza sababu nyingine za ugonjwa huo, bi Malugu alisema kuwa, kuwa na wanaume wengi na hata kuwa na watoto wengi ni sababu nyingine ya kupata saratani hiyo kwa mujibu wa wataalamu.
Nae mwakilishi kutoka wizara ya Afya bi Lotalis Gadau, alisema kuwa kutibiwa saratani ya shingo ya kizazi gharama yake ni milioni tano na laki tano, ambayo ni gharama kubwa sana hivyo aliwasihi sana wanakijiji wa mang’ula na maeneo yote ya wilaya ya Kilombero kupata chanjo hii mapema kabla tatizo halijakuwa kubwa kwani chanjo ni bora kuliko tiba.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa