WAKATI mvutano Wa kugombea kijiji cha Ngombo ukiendelea baina ya wilaya mbili za Kilombero NA Malinyi,wajumbe Wa kamati ya ushauri(DCC) Wilaya ya Kilombero kwa kauli moja wamesema mipaka inayotambulika kiserikali iheshimike kwa kijiji hicho kuonekana kipo Wilaya ya Kilombero.
Wakizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya,wajumbe hao walisema wanashangaa ofisi ya Mkuu Wa mkoa kuendelea kulikumbatia suala hilo wakati wakielewa katika ramani inaonyesha kuwa eneo la kijiji hicho lipo ndani ya Wilaya yao.
Akiwasilisha ajenda hiyo kwa wajumbe,mwenyekiti Wa kikao hicho ambae ni Mkuu Wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo alisema kuwa ameagizwa NA ofisi ya Mkuu Wa mkoa kuanza kuchukua upya maoni Wa wajumbe Wa Wilaya ili wao wakikutana katika kikao cha Rcc wapokee maoni ya pande zote mbili kisha kutoa maamuzi.
Ihunyo alisema mwaka uliopita Mkuu Wa mkoa aliitisha kikao cha kamati ya ulinzi NA Usalama NA viongozi Wa Wilaya zote mbili ili kulijadili suala hilo lakini wajumbe Wa Wilaya ya Malinyi hawakutokea hivyo kuagiza wajumbe Wa DCC kulijadili suala hilo.
Hivyo aliwataka wajumbe kutoa ushauri ukizingatia kuwa mipaka toka Tamisema inaonyesha kabisa kuwa eneo hilo lipo ndani ya Wilaya ya Kilombero licha ya wananchi wake kupata Huduma muhimu wilaya ya Malinyi.
Katibu Wa chama cha mapinduzi(Ccm) Wilaya ya Kilombero Bakari Mfaume alisema kuwa kimsingi eneo lipo wilaya ya Kilombero NA mamlaka za wilaya ya Kilombero zilichangia eneo hilo kuchukuliwa NA iliyokuwa wilaya ya Ulanga kabla ya kugawanywa NA kuwa wilaya mbili za Ulanga NA Malinyi .
Mfaume alitaja sababu zilizochangia eneo hilo kuchukuliwa ni kutopeleka Huduma za kijamii kwa muda mrefu NA hali hiyo ilipelekea wananchi Wa eneo hilo kujiona wapo wilaya ya Ulanga NA kupelekea kuwa NA Mtendaji NA mwenyekiti wanaotambulika wilaya mpya ya Malinyi .
Ameishauri serikali kupitia halmashauri ya wilaya ipeleke watendaji NA ikiwezekana uitishwe uchaguzi eneo hilo ili kweli wananchi wawe NA imani kuwa wilaya yao inawajali NA wakiruhusu eneo hilo liende Malinyi kuna hatari maeneo mengi yaliyopo pembezoni yatachukuliwa.
Naye mwenyekiti Wa Chama cha demokrasia NA Maendeleo(Chadema) wilaya ya Kilombero Shabani Mikongolo alisema mipaka iliyowekwa iheshimiwe NA kama wananchi wanahudumiwa wilaya ya Malinyi sio hoja NA kusema kuwa mbona watu Wa kata ya Uchindile ipo wilaya ya Kilombero lakini Huduma zote za kijamii wanazipata eneo la Mufindi lakini wao wanahesabika wapo Kilombero.
Mikongolo amewataka wajumbe Wa kikao cha ushauri cha mkoa(Rcc) ambacho kitaa hivi karibuni waheshimu mipaka inayotambulika NA watoe maamuzi haraka iwezekanavyo ili halmashauri ipeleke watendaji eneo hilo.
Mwisho....
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa