Pichani juu: Greda ikiendelea kuchonga barabara katika eneo hilo.
Eneo lililotengwa kwaajili ya upimaji wa viwanja katika eneo la Itongoa, tayari limeanza marekebisho kwa kuanza kuchonga barabara tayari kwaajili ya mauzo kwa wananchi waliochukua fomu za manunuzi ya viwanja hivyo.Akizungumzia kuhusiana na viwanja hivyo, mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba mhandisi Stephano Kaliwa amesema kuwa viwanja hivyo ni moja ya miradi ya Halmashauri ambayo ina lengo la kuwasaidia wananchi kurasimisha Ardhi wanazozimiliki kwani walikaa kikao na wananchi na kuzungumzia suala hilo kabla ya kuamua kupima maeneo hayo na kugawana na wananchi waliokuwa wanayamiliki maeneo hayo kabla.Katika hatua nyingine mhandisi kaliwa amesema kuwa ili kuhakikisha wanatengeza mazingira yaliyo salama kwa viwanja hivyo, Halmashauri imeamua kutengeneza Barabara, ambapo ndani ya mradi huo kutakuwa na soko, kituo cha polisi, maeneo ya wazi na vivutio vya kula aina ili kuweza kufanya eneo hilo kuwa la kisasa Zaidi na kuwavutia watu wengi Zaidi kuweza kuyafikia maeneo hayo kwa urahisi.Nae Afisa Ardhi mteule Ndg Remigius Lipiki amesema kuwa maeneo ya kununua bado yapo mengi hivyo amewashauri wananchi kutoka maeneo mbalimbali kufika katika ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Mlimba zilizopo maeneo ya Itongoa ili kuweza kuchukua fomu kwa gharama ya shilingi Alfu Ishirini tu, kisha kukabidhiwa kiwanja chake ambacho atakilipia kwa kuzingatia ukubwa wa eneo analolihitaji na kwa nafasi atakayokuwa nayo ili kuweka mazingira safi ya upatikanaji wa viwanja hivyo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa