Pichani juu: Gari ya Halmashauri ya wilaya ya Mlimba ikiwa imebeba Matumba hayo ya samaki ambayo yamekamatwa mapema jana jioni.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa amesema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero mapema Jana imekamata matumba ya samaki yapatayo matano (5) pamoja na baiskeli mali ya wachuuzi wa maeneo ya Mofu, katika shughuli za kawaida kabisa za doria katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Akizungumza kwa uchungu kabisa Mhandisi Kaliwa amesema kuwa mitumba hayo ya samaki yangeweza kuipatia Halmashauri kiasi kadhaa cha pesa ambazo zingesaidia kufanya maendeleo kwa wananchi wenyewe.
Aidha Mhandisi Kaliwa amesema kuwa Matumba hayo ya samaki yamekamatwa kwa wachuuzi hao ambao walikuwa katika harakati za kujaribu kuyatorosha kwa njia za magendo pasipo kufata utaratibu uliowekwa na serikali wa kulipa kodi pamoja na kukata Leseni za biashara hiyo.
Akiongea Zaidi Mhandisi kaliwa amesema kuwa wapo watu wengi sana ambao huamua kufanya biashara za magendo hivyo hawa waliokamatwa wwatakata Leseni, pamoja na kulipa faini kali ili iwe fundisho kwa wengine, amesema kuwa lengo si kuwalipisha faini bali ni kuwakumbusha watu wafate utaratibu katika kufanya biashara zao ili kuepuka usumbufu wa kukamatiwa mali zao na hatimae kuua mitaji yao ya biashara, kwani wengine wanategemewa kurejesha mikopo waliyochukua kwaajili ya biashara hizo.
‘’Wapo watu wengi sana ambao kwa makusudi kabisa, huamua kufanya biashara za magendo, hivyo kwa hawa waliokamatwa watakata leseni na kulipa faini kali ili iwe fundisho kwa wengine, ingawa ieleweke wazi kuwa lengo si watu kulipishwa faini na Halmashauri yetu, bali ni kukumbushwa kuwa wanatakiwa kufanya biashara zao kwa kufuata utaratibu kuepukana na kukamatiwa biashara zao na kisha kuua mitaji yao ya biashara kwani wengine wamekopa pesa na wanategemewa kurejesha mikopo hiyo’’ Alisema Mhandisi Kaliwa.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa