Pichani juu: Bwana Yuki Mito, Afisa maendeleo ya jamii wa kujitolea Kilombero, kutoka JICA, akiongea na baadhi ya wateja waliotembelea, kwenye kizimba chake mapema leo katika banda la maonyesho la Nanenane.
Wakaazi wa Morogoro mapema leo wameendelea kumiminika na kupata habari kadhaa zinazohusiana na kilimo na Ufugaji.
Akiendelea kuzungumza na wateja hao, Afisa maendeleo ya Jamii kutoka JICA, ambaye anafanya kazi katika kata ya Mang’ula, Bwana Yuki Mito amesema kuwa, hakika kazi imekuwa ngumu kwani amepokea wateja wengi na amefanya biashara yake ya kuuza vipepeo kwa wingi sana.
Aidha katika hali nyingine wateja wamesema kuwa, amekuwa kivutio kikubwa sana, kutokana na namna ambayo amekuwa akizungumza Kiswahili fasaha ingawa alikuwa akitumia lafudhi ya kikwao ya Japani.
Pia pamoja na bwana Mito lakini pia, biashara imekuwa nyepesi kwa wataalamu wote waliokuwa katika maonyesho hayo wamesema kuwa wameridhishwa mno na kasi ya uingiaji wa wananchi wa Kilombero katika banda hilo, na kusema kuwa wamefurhishwa sana na kasi hiyo na hivyo kuwatia moyo kurejea tena wakati mwingine wa Nanenane kwani angalau hata wameweza kupata pesa kiasi kwa kuuza bidhaa zao.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa