Pichani: Kushoto ni Ndg Francis Ndulane, mkurugenzi wa mji ifakara pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero Ndg Dennis Londo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Kilombero Ndg Dennis Londo na mkurugenzi wa mji mdogo Ifakara Ndg Ndulane wametakiwa kushirikiana kuhakikisha kuwa kitongoji cha Mbasa kilichopo Ifakara kinapatiwa Umeme wa uhakika.
Akijibu kero za wananchi kwenye mkutano na wana kitongoji wa Mbasa hapo jana alipotembelea kwenye kitongoji hicho kukagua miradi kadhaa iliyotekelezwa na serikali ya awamu ya awamu ya tano, bwana Humphrey polepole ambaye pia ni katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi alisema kuwa, kuna kila sababu ya wanakijiji hao kuweza kupata haki yao hiyo ya msingi kwani, ukosefu wa umeme ni kikwazo kikubwa sana cha maendeleo.
Aidha aliwaagiza wakurugenzi hao kuhakikisha kuwa katika bajeti zao wanakipa kipaumbele kitongoji hicho ili kuhakikisha kinapatiwa huduma hiyo muhimu sana kwa maendeleo ya wanadamu.
Katika kuonyesha kuwa wamelipokea na kulifanyia kazi suala hilo, wakurugenzi hao kwa pamoja waliahidi kulifanyia kazi suala hilo kwa kushirikiana na Tanesco ili kuweza kukidhi kiu ya muda mrefu ya wanakitongoji hao.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa