Pichani baadhi ya walimu wakichukua vitabu vya kufundishia na kujifunzia mapema jana katika ofisi ya vifaa na takwimu kwa shule za msingi kwa halmashauri ya wilaya kilombero.
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero mapema wiki hii imepokea vitabu vya Elimu ya msingi kwa Mtaala mipya kwa shule zote za Msingi zilipo wilayani kilombero.
Kaimu Afisa Elimu Msingi Vifaa na Takwimu wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero ndugu Saidi Kivufu amesema, wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi ikiwa inalengo la kuboresha elimu kupitia mitaala mipya, imeamua kuleta vitabu hivyo ili kuleta ufanisi katika kipindi hiki cha harakati za upatikanaji wa elimu bora, ambapo vitabu hivyo ni kuanzia darasa la kwanza, la pili na darasa la tatu vitabu vitakavyotumika kufundishia na kujifunzia kupitia mitaala mipya kwa shule zote za Msingi kitaifa.
Katika hatua nyingine bwana kivufu amesema kuwa, mpaka sasa vitabu vilivyokwishapokelewa na halmashauri ya wilaya ya kilombero ni 43063 ambapo Kwa darasa la kwanza na Darasa la Pili vitabu vilivyopokelewa ni vya Michezo na Sanaa, Afya na Mazingira na vile vya kusoma na kuandika, wakati kwa Darasa la Tatu vitabu vilivyopo ni Maarifa ya Jamii na English.
Hata hivyo mpaka sasa tayari Wakuu wa Shule za Msingi wamekwishapokea vitabu hivyo kutoka kwenye ofisi ya vifaa na takwimu ya halmashauri ya wilaya ya kilombero tayari kwa kutumia mashuleni.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa