Pichani juu: mkuu wa wilaya ya Kilombero ndg James Ihunyo akiongea na wananchi wa mngeta juu ya
MKUU Wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo amesema kuwa viongozi wote waliohusika kuwauzia wananchi Mashamba katika eneo la Pori tengefu la Kilombero wilayani humo watafunguliwa mashtaka.
Kauli hiyo ameitoa Jana katika kata ya Mngeta wakati akizungumza na viongozi Wa vijiji,vyama vya siasa na wananchi katika ziara yake ya kuzungukia na kuhimiza shughuli za Maendeleo katika Wilaya hiyo.
Ihunyo amesema kwa sasa tatizo kubwa lililopo wilayani humo ni ardhi na hiyo inatokana baada ya serikali kuamua kupima mipaka ya vijiji vilivyotengana na pori tengefu na kubainika kuwa wananchi wengi waliovamia maeneo hayo waliuziwa na baadhi ya viongozi.
"Changamoto kubwa hivi sasa kilio cha ardhi baada ya serikali kupima maeneo yenu,tunafahamu wengi wenu mlivamia maeneo hayo lakini kuna wengine waliuziwa maeneo hayo na baadhi ya viongozi wenu,"alisema Ihunyo.
Amebainisha kuwa kwa sasa serikali baada ya kupima vijiji vilivyopo Jirani na pori tengefu wamebaini baadhi ya viongozi waliopo madarakani ama waliostaafu wameleta usumbufu baina ya serikali na wananchi kwa kuuza maeneo yasiyoruhusiwa hivyo serikali haitafumbia macho suala hilo.
Amesema viongozi Wa namna hiyo ni matapeli kwani wanaelewa eneo hilo ni mali ya serikali hivyo kuwataka viongozi waliopo madarakani kufuata taratibu na Sheria lasivyo mkono Wa Sheria utahusika upande wao.
Hata hivyo Mkuu huyo Wa Wilaya amesema katika utafiti uliofanyika hivyo karibuni umebaini kaya 248 katika vijiji vitatu katika tarafa ya Mngeta zimeathirika baada ya kuonekana zinaishi katika eneo chepechepe kwa miaka mingi na serikali zitawatafutia maeneo mengine ya makazi.
Amesema kaya 219 zipo kijiji cha Igia,kaya 18 zipo kijiji cha Isago na kaya 11 zipo kijiji cha Luvilikila na wahusika walijenga makazi ya kudumu katika maeneo hayo na zoezi la kutafuta wahusika wengine likiendelea.
Kuhusu baadhi ya wakulima wakubwa ambao wapo nje ya Wilaya wanamiliki maeneo makubwa ya ardhi na kutoyaendeleza,Ihunyo alisema serikali ipo katika hatua za mwisho za kubaini suala hilo na ikibaini hawayaendelezi na hawakupata kihalali serikali haitosita kuyapora na kuyarudisha kwa wananchi.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa