Pichani juu: Mkuu wa wilaya ya Kilombero Ndg James Ihunyo akizungumza na wakazi wa kijiji cha Msolwa
MKUU Wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo amesitukua mtego aliowekewa na wakazi Wa kijjji cha Msolwa Stesheni waliotaka Mkuu huyo awaruhusu kuwakamata na kuwapeleka kwa mganga wale wote wanaohisiwa uchawi katika kijiji hicho.
Tukio hilo la aina yake limetokea Jana baada ya wakazi Wa kijiji hicho kupiga kura za siri za kuwabaini wachawi ambao wanahisiwa kusumbua wanafunzi wa kike Wa shule ya msingi Kibong'oto kupatwa na mapepo na wanafunzi 24 wamekumbwa na mapepo na kuibua hali ya sintofahamu katika kijjji hicho.
Baada ya kutokea kwa mapepo hayo kwa wanafunzi ndipo ulipoitishwa mkutano Wa kijiji na wananchi kudai kuwa kuna wazee ambao ndio wanasumbua wanafunzi hao na kutaka kupiga kura za siri ili kuwataja na hatimae walipiga kura za siri za kuwataja.
Kilichofuata sasa ni kupewa kibali na kijiji ili wawakamate na kuwapeleka kwa mganga Wa jadi aitwae Bibi Kalembwana, ili kunyolewa na hatimae kutolewa uchawi, ingawa zoezi hilo lilishindikana kwa viongozi wa kijiji kuhofia kuvunjika kwa amani kijijini hapo hatimae kulifikisha suala hilo kwa Mkuu Wa Wilaya ili kulipatia ufumbuzi.
Akihutubia mamia ya wananchi waliokuwa na shauku ya kupata kibali kutoka kwa Mkuu huyo Wa wilaya,Ihunyo alipotoa nafasi ya kuwasikikiza wananchi kila Mwananchi aliyeinuka alimweleza Mkuu huyo wa wikaya kuwa njia pekee ya kuondoa tatizo kwa wanafunzi hao ni kuruhusu wahusika wakamatwe na kisha kupelekwa kwa bibi kunyolewa na ndipo tatizo hilo litamalizika kijijini hapo.
Naye Mwenyekiti Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero David Ligazio, aliwasihi wananchi hao kuwa tatizo hilo wanaweza kulimaliza wenyewe bila kupelekana kwa bibi, hivyo kuwaomba wanaofanya kitendo hicho kuwaonea huruma watoto hao, na kama hali ikiendelea hivyo kuna hatari shule kufungwa na watoto kukosa masomo.
Licha ya maelekezo kutoka kwa viongozi Wa wilaya na Wa dini asilimia kubwa ya wananchi walitaka wahusika wakamatwe na kupelekwa kwa bibi, kwani wanajulikana na kutamba kuwa hamna MTU ataewafanya lolote na atakaejipendekeza kwao nae watamdhuru.
Baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote ndipo Ihunyo alipotoa maamuzi kuwa, serikali haitaruhusu mtu yeyote kukamatwa na kupelekwa kwa bibi kunyolewa kwa kisingizio cha uchawi na yeyote atakaethubutu hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Ihunyo alisema, serikali haitambui uchawi na kama suala hilo likiruhusiwa litaleta madhara katika kijiji hivyo kuwaomba wazee na viongozi Wa dini wasaidie ili matatizo hayo yaishe.
Awali akitoa taarifa ya tatizo la mapepo kwa wanafunzi Wa kike shuleni hapo, Afisa Mtendaji Wa kata ya Msolwa Stesheni Joachim Lyembela alisema, lilianza kwa mwanafunzi mmoja Wa darasa LA saba akiwa kwenye mtihani Wa kujipima Wa kata hapo Machi mwaka huu.
Lyembela alisema Juni mwaka huu tatizo liliendelea na kadri siku zinasonga tatizo hilo kuongezeka na wanafunzi wanaokumbwa na mapepo ni Wa kike kuanzia darasa la nne hadi la saba na hali hiyo imepelekea shuleni hapo kukosekana amani na walimu kushindwa kufundisha kwa wiki tatu sasa.
Mtendaji huyo amebainisha kuwa wanafunzi wanaotokewa na mapepo, wamekuwa wakiingia ofisini na kufanya vurugu na kuwakaba wanafunzi wengine, na kufanya wanafunzi wengine kuogopa kufika shuleni na hadi sasa wanafunzi 24 wametokewa na mapepo na wengine zaidi ya 30 huwatokea siku moja moja kutoka madarasa tofauti.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa