Pichani juu: Wananchi wa Idete wakizungumza na mkuu wa wilaya ya kilombero ndg Jmes Ihunyo.
SERIKALI wilayani Kilombero imetoa tahadhari kwa wananchi kuacha kurubuniwa na wafanyabiashara ili kusafirisha mazao yao na kukwepa kulipa ushuru kwa madai ya kutekeleza agizo LA Rais la kutolipia ushuru Wa mazao.
Akizungumza na wananchi Wa kata ya Idete wilayani humo mapema jana,Mkuu Wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo amesema agizo LA Rais Magufuli ni kutaka wakulima wenye mazao yasiyozidi tani moja kupita bure katika vizuizi na kutolipia ushuru na sio kuzudisha mzigo na pia kusafirisha mazao ya wafanyabiashara.
Wakati akiwa katika ziara wilayani Kilombero hivi karibuni,Rais Magufuli alirudia agizo kuwa ni marufuku kwa wakulima kutozwa ushuru kwa mazao yasiyozidi tani moja na kiongozi yeyote atakaekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua ikiwezekana kutuliwa kazi.
Hata hivyo kumekuwepo na tuhuma za baadhi ya wafanyabiashara kwa kushirikiana na wakulima kusafirisha mazao hayo na kudai kuwa mazao ya wakulima na njia hiyo upelekea kuzikosesha halmashauri Fedha za ushuru.
Ihunyo alisema ni marufuku wakulima kushirikiana na wafanyabiashara hao kusafirisha mazao hayo na punde ikibainika wahusika wote watachukuliwa hatua ikiwemo kupigwa faini na kusisitiza kuwa mkulima hatolipia mzigo Wa chini ya tani moja na mazao yakiwa ya kwake tu.
Amebainisha kuwa zaidi ya tani moja mkulima lazima alipie ushuru ili kuipatia halmashauri Fedha za kuwaletea wananchi shughuli mbalimbali za Maendeleo.
Amesema kwa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero ilijiwekea utaratibu Wa kutambua wakulima wake kwa kuwapa vibali maalum baada ya mavuno na njia hiyo usaidia kusafirisha mazao yao bila usumbufu ila kuna baadhi ya wajanja utumia mbinu mbadala kwa kusafirisha mazao na kukwepa ushuru.
Aidha Mkuu huyo Wa wilaya amewataka watendaji kushirikiana na wananchi katika kuwatambua na kuwabana wafanyabiashara walanguzi wanaokuja na ndoo kubwa katika kununua mpunga huko mashambani na kusema njia hiyo ni kumnyonya mkulima.
Kwa sasa baadhi ya maeneo baada ya kubaini wakulima wanavuna mpunga baadhi ya walanguzi wameingia mashambani na kuwarubuni wakulima na kununua mpunga mashambani kwa kutumia ndoo zilizopigwa marufuku wakati vipimo vinavyotambulika na serikali ni mizani.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa