Pichani ni Mratibu wa mradi wa shirika la children in Crossfire ndugu Frank Samson akitoa mafunzo kwa baadhi ya waratibu wa elimu kata na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero.
Shirika lisilo la kiserikali la Children in Crossfire mapema jana imehitimisha mafunzo kwa waratibu wa elimu wa kata wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero na kusisitiza mambo mengi muhimu ya kuwafanyia wanafunzi hususan watoto kwenye suala la elimu jumuishi na mazingira ya ufundishaji kwa ujumla.
Shirika hilo limechukua hatua hiyo kutokana na ukweli kwamba, mazingira ya watoto hao yamekuwa katika hatari kubwa na kusababisha matatizo mengi kwa watoto hao.
Akizungumza juu ya suala la elimu jumuishi, mratibu wa mafunzo hayo wa shirika hilo lenye makazi yake jijini Dar es salaam bwana Frank Samson amesema kuwa elimu jumuishi ni aina ya elimu ambayo inawaweka pamoja watoto wenye na wasio na uhitaji maalum ndani ya darasa moja na kujifunza bila kujali hali, mwonekano na historia yake au ya jamii.
Aidha bwana Samson alisisitiza kuwa watu ambao wanahitajika kujumuishwa kwenye elimu hiyo jumuishi ni wenye ulemavu wote, wanaoishikatika mazingira magumu, wenye magonjwa ya kudumu, wenye msongo wa mawazo, waliokataliwa na wazazi, wanaotoka kwenye familia zilizotengana na wale watoto wote ambao ni wazima kabisa.
Pamoja na hayo yote pia aligusia juu ya suala la mikakati jumuishi kuwa ni lazima kujua historia na uhitaji wa kila mtoto, mpangilio bora na mzuri wa darasa pamoja na kuweka mbinu shirikishi za ufundishaji darasani ni njia moja wapo ya mikakati hiyo.
Akimalizia mafunzo hayo, meneja mradi wa shirika hilo ndugu Heri Ayoub alisema kuwa kwa sasa umefika wakati kuwa tuweke maazimio kutokea chini kwenye kata zetu, kuona ni namna gani watoto hawa wanaweza kukumbukwa na kusaidiwa kutimiza malengo yao katika suala zima la kielimu masuala mengine yote yanayowahusu.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa