Pichani juu: Mkuu wa wilaya ya Kilombero ndugu James Ihunyo (Aliyeshika funguo) akimkabidhi funguo hizo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero ndugu Daudi Ligazio (Mwenye Miwani) kama ishara ya kukabidhi Pikipiki Ishirini zilizotolewa na TAMISEMI kwaajili ya waratibu wa elimu kata wa Halmashauri hiyo.
Mkuu wa wilaya ya kilombero James Ihunyo mapema leo amemkabidhi mwenyekiti wa halmashauri ya kilombero ndugu Daudi Ligazio jumla ya Pikipiki ishirini kwaajili ya uboreshaji wa kazi za kielimu katika kata zote za halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Akizungumza na waratibu hao ndugu Ihunyo alisema kuwa pikipiki hizo zimetolewa na serikali kwaajili ya shughuli za kiserikali tu, na kwa hali hiyo basi ni vema ikiwa zitatokea shughuli za kibinafsi, basi pikipiki hizo zikaachwa ili isije kutokea tatizo kwenye shughuli zisizotarajiwa.
Nae mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya kilombero, ndugu Dudi Ligazio akiwaasa alisema kuwa, katika kutumia Pikipiki hizo wanatakiwa kuwa makini sana, kuepuka ajali za mara kwa mara, hukuakitoa mifano ya Pikipiki kadhaa za Halmashauri zilizopata ajali na kuharibika kwa kiwango kikubwa sana na hata kupelekea kuwaacha watumishi katika hali ya majeraha.
Akitoa shukrani kwa serikali, mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero alisema kuwa, anaishukuru sana serikali ya jamhuri ya muungano kupitia wizara ya TAMISEMI, kuwa ile ndoto ya siku nyingi ya kuhitaji usafiri imetimia, hivyo akawaahidi serikali kuwa atasimamia kwa umakini Pikipiki hizo ili kuhakikisha kwamba lengo lililotarajiwa kufikiwa kwa matumizi yake, litimie.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa