Pichani juu: Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Dr. Christina Guveti, akizungumza jambo na wananchi kusisitiza chanjo hiyo.
JUMLA ya watoto wapatao 44,500 wanatarajia kupata chanjo ya Surua Rubella katika halmashauri ya wilaya ya Kilombero katika zoezi litakaloanza Oktoba 17 hadi 21 mwaka huu.
Sambamba na utoaji huo Wa Surua Rubella pia watoto wapatao 25747 wanataraji kupata chanjo ya Polio ya sindano katika zoezi hilo.
Mratibu Wa chanjo katika halmashauri hiyo Niindaely Malugu amesema kampeni hiyo itahusisha vituo vyote 49 vinavyotoa chanjo katika halmashauri hiyo na vituo vingine vya huduma za mkoba ambavyo chanjo huwa inatolewa.
Malugu amesema zoezi hilo ni kutekeleza agizo la wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia,wazee na watoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Amesema kampeni hiyo imelenga kutoa chanjo kwa watoto wote walio na umri kuanzia miezi 9 hadi chini ya miaka mitano kwa chanjo ya Surua Rubella na watoto walio katika umri Wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na nusu watapatiwa chanjo ya polio ya sindano.
Amebainisha kuwa watoto watakaopatiwa chanjo ya polio ya sindano ni wale waliozaliwa mwezi April 2016 hadi April 2018 hivyo kutoa wito kwa Wazazi kuwapeleka watoto wao waliozaliwa kipindi hicho.
Akielezea sababu zinazochangia kampeni hii kufanyika,Malugu alisema kuwa kuna uthibitisho wa kitaalamu kwamba ni asilimia 85 tu ya watoto wanaopata chanjo ya surua wakati wanatimiza miezi 9 .
Amesema kwa halmashauri hiyo takwimu zinaonyesha kuanzia Januari 2017 hadi Agosti 2019 watoto wapatao 6237 hawakupata chanjo ya Surua Rubella dozi ya kwanza na watoto wapatao 3900 hawakumaliza kupata chanjo hiyo dozi ya pili.
Kwa upande wake Mganga Mkuu Wa halmashauri hiyo Dk Christina Guveti amesema lengo mahususi la kampeni hiyo kitaifa ni kuzuia na kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo na pia kuongeza kinga kwa watoto wote kwa kuwapatia chanjo hata kama walishapata chanjo siku za nyuma.
Naye Mkuu Wa Wilaya hiyo James Ihunyo ametoa wito kwa wananchi hasa Wazazi na walezi kuhakikisha watoto Wa umri chini ya miaka mitano wanapatiwa chanjo hizo na kuwataka viongozi Wa kijamii,madhehebu ya dini kuhamasisha Jamii ili kufanijisha zoezi hilo.
Mwisho,...
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa