Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Eng. Stephano B. Kaliwa kwa kuandaa Bonanza la Michezo kwa watumishi wote ambalo limefanyika Kata ya Chita leo Jumamosi tarehe 24/02/2024.
Mtendaji kata wa Idete Bi. Janneth Tuji amesema kufanyika kwa Bonanza hilo katika kata yake kumehasisha zaidi watumishi wa kata ya Chita kwani hakujawai tokea Bonanza kubwa na nzuri kama hilo, pia amemshukuru Mkurugenzi kwa kuwahamsisha watumishi kupitia Michezo kwani inawasaidia kupunguza msongo wa mawazo, kuimarisha Afya zao pamoja na kuwajengea mshikamano watumishi wote wa Halmashauri.
Pia, Mheshimiwa Asha Shomary ambaye ni Diwani wa kata ya Chita awewapongeza watumishi wote walioshiriki Bonanza hilo na kuwaasa wacheze kwa kulindana na kuepusha kupata changamoto za majeraha wakati wa Michezo aidha amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kuandaa Bonanza hilo na ameomba lifanyike kila Mwezi kwa kata tofauti ili watumishi wote wa Halmashauri wawe vizuri kiafya.
Mwalimi Joyce Gabriel amesema amevutiwa zaidi na mbinu ya Kuwashirikisha watumishi wote kushiriki Bonanza na kuonesha Vipaji walivyo navyo watumishi nje ya Taaluma zao. Amemuomba Mkurugenzi Bonanza hili liwe mara kwa mara kufanya kila Mtumishi wa Halmashauri kujifunza mazingira mbalimbali ya Halmashauri na kutambua fursa zilizopo.
Mwisho, Afisa Michezo wa Halmashauri Ndugu Nicholaus Makata amewapongeza watumishi wote kutoka Kata mbalimbali kushiriki na kuitikia Wito wa Bonanza na amesema huu ni utaratibu wa Halmashauri kufanya Mabonanza ya Michezo kwa kila kata na yatafanyika kila Mwisho wa Mwezi ili kuendelea kuimarisha Afya za Watumishi pamoja na kujiandaa katika Mashindano mbalimbali ya Watumishi kama vile @shimisemita_taifa au ligi mbalimbali zitakazoandaliwa ndani ya Halmashauri.
Matokeo ya Michezo iliyofanyika leo ni Mpira wa Miguu watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri wamewafunga watumishi wa Kata ya Chita Goli Moja bila na Mchezo wa Netiboli watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri wameshinda goli 12 dhidi ya Goli 4 za watumishi wa kata ya Chita. @kyobyad @dc.kilombero @jr_farhanjr @hajathecredible @yahyanjenge @godwin_kunambi
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa