Pichani juu: waziri mkuu Mh: Kassim Majaliwa Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero na wa Mji Ifakara
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi wa Halmashauri za Kilombero na Ifakara Mji Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro kwa tuhuma za ubadhilifu wa zaidi ya Tsh. 1.3 Bil.
Mhe. Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi hao Kuanzia jana Jumapili, Septemba 15, mwaka huu wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri hizo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero uliopo kibaoni.
Aidha pamoja na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu amewataka watumishi hao wanaotuhumiwa, kurejesha fedha wanazotuhumiwa nazo kabla hajamaliza ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Watumishi wanaotuhumiwa na sakata hilo ni pamoja na Reina Mrema ambaye anadaiwa kuchukua kiasi cha sh. milioni 298, Haile Njitango milioni 73, Linus Mdembo kiasi cha sh. milioni 2 kwa kushirikiana na Gregory Midas ambaye ni mtendaji Kata wa viwanja Sitini katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara.
Kuhusu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bwana Francis Ndulane ambaye ametuhumiwa kuingiziwa fedha kiasi cha sh. milioni Tano (5,000,000) katika akaunti yake binafsi huku akitaja tarehe pamoja na akaunti iliyoingizwa pesa hiyo, Waziri Mkuu ameagiza fedha hizo zirudishwe mara moja ikiwa ni kweli zimechukuliwa huku akitakiwa kukabidhi stakabadhi ya marejesho hayo kwa Waziri Mkuu kabla hajamaliza ziara yake mkoani morogoro.
Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi juni 2019, Katika mji wa Ifakara makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7 ambapo fedha iliyopelekwa banki ni shilingi bilioni 1.9 na kufanya kiasi cha shilingi milioni 727 kutokuwa na maelezo ya kutosha juu ya matumizi yake na mahali ilipopelekwa.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa