Pichani juu Kaimu Mkurugenzi wakili Faraja Nakua akimkabidhi funguo ya pikipiki moja kati ya wauguzi wanaofanya kazi wilaya ya Mlimba.
Wauguzi katika Halmashauri ya wilaya ya Mlimba mapema jana wamekabidhiwa pikipiki na shirika lisilo la kiserikali la PLAN INTERNATIONAL kwa madhumuni ya kurahisihsha utendaji kazi wao katika maeneo ambayo hayafikiki kwa magari, kwenye hafla fupi iliyofanyika katika makao makuu ya Halmashauri ya wilaya hiyo.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhiwa pikipiki hizo,kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Wakili, Faraja Nakuwa amesema kuwa, malengo ya pikipiki hizo ni kuwasaidia wauguzi kutimiza malengo ya kiutumishi ambayo ni kuwafikia kwa urahisi wahitaji wa huduma mbali mbali za kiafya hususani wamama wajawazito na watoto walio chini ya miaka mitano na kuongeza ufanisi wa kazi wanazozifanya.
Katika hatua nyingine, Meneja miradi wa Plan International Program ya Ifakara Ndugu Silvin Masele amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na uongozi wa wilaya hiyo kwani wameridhishwa na utendeji kazi wa watendaji katika ngazi ya wilaya kwa kutekeleza miradi mingi wilayani humo.
Nae Verediana Martine ambae ni miongoni mwa wanufaika wa pikipiki hizo akihudumu katika zahanati ya Mbingu amesema kuwa wanashukuru sana shirika hilo kwani kwa kukabidhiwa pikipiki hizo kutawarahisishia kazi, kwani walikuwa wakipitia changamoto ya kuwafikia wananchi, lakini kwa sasa wana uwezo wa kuwafikia watu wote.
“kusema ukweli tunamshukuru mungu na Plan kwa kutupatia pikipiki hizi ambazo zitaenda kurahisisha kazi kwani tulikuwa tunapitia changamoto kubwa sana ya usafiri hivyo kwa sasa tunauwezo wa kuwafikia karibia watu wote na kuwapa huduma.’’ Alimaliza Martine.
Naye Julius Jumanne ambae ni mtoa huduma wa tiba chanjo wa wilaya, amewataka wadau wengine wa maendeleo kujitokeza ili kuuunga mkono juhudi zinazofanwya na serikali kama walivyofanya shirika la Plan International Wilayani Mlimba.
Shirika la Plan International limekuwa likitekeleza miradi mbalmbali katika wilaya zilizopo mashariki mwa mkoa wa Morogoro na hatimaye awamu hii wameweza kutoa pikipiki takribani 18 ambapo pikipiki 16 zimegawiwa kwa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba na mbili zimeenda katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara.
Habari picha
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa