Pichani juu: baadhi ya wavuvi wakikata leseni zao kwa kutumia Poss za Halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Kambi ya uvuvi ya mbuti iliyopo kata ya ziginari katita halmashauri ya wilaya ya Kilombero jana imefanikiwa kukata leseni mpya za uvuvi 54 zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni mbili (2,000,000/=) kutokana na ushawishi mkubwa uliofanywa na maafisa uvuvi wa kata na viongozi wengine wa wilaya.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi wa halmashauri ya wilaya ya kilombero Dr. Annete Kitambi amesema kuwa kupatikana kwa kiasi hicho ni matokeo ya utoaji wa elimu wa hali ya juu kwa wavuvi hao.
Aidha Dr. Kitambi alisema kuwa wiki iliyopita walikamatwa watu kadhaa ambao walikuwa na samaki pasipokuwa na leseni ambao walichukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kulipishwa faini, ambapo njia hiyo ilipelekea wavuvi wengi kuchukua hatua ya kukata leseni kwaajili ya shughuli zao hizo kwa njia ya halali.
Katika kuhamasisha zaidi Dr. Kitambi alisema kuwa wavuvi wote wanaofanya sghughuli zao katika halmashauri ya wilaya ya kilombero, wahakikishe kuwa wanakata leseni zao ili kujiweka katika mazingira salama ya ufanyaji kazi na kuepuka usumbufu wowote unaoweza kujitokeza kuzuia shughuli zao, ikiwemo kupiga mnada samaki wote watakaopatikana ima kwa kuvuliwa katika eneo la Halmashauri au kwa kununuliwa na wafanyabiashara wasio na leseni.
‘’wavuvi wote mnatakiwa kuvua kwa kufuata sheria kwa kuvua kwa nyavu zinazokubalika kihalali na samaki wenye ukubwa unaokubalika kisheria, na ikiwa itafanyika vyovyote kinyume na utaratibu huu, basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kesi kwa mujibu wa sheria.’’ Alimaliza Dr. Kitambi.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa