Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa amesema wazazi ambao hawajapeleka watoto shule kujiunga na darasa la Awali, darasa la Kwanza na waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza watachukulia hatua kali za kisheria kwa sababu wanawanyima watoto wao haki ya kupata elimu.
Mhe. Fatma Mwassa ametoa tamko hilo January 23 mwaka huu wakati akifungua kikao kazi cha Viongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri kilichofanyika katika hoteli ya Morena iliyopo Manispaa ya Morogoro.
Mhe. Fatma Mwassa amesema Serikali ya Awamu ya Sita imewekeza fedha nyingi kwa ajili ya kujenga miundombinu ya madarasa, vyoo pamoja na madawati lakini hadi sasa ni asilimia 45 ya wanafunzi walioripoti shuleni na bado kuna idadi kubwa ya watoto walio majumbani ambao hawajaenda Shuleni na wazazi wamekuwa wakitoa sababu kuwa hawana fedha ya kukidhi mahitaji ya sare kwa wanafunzi.
Aidha, Mhe. Fatma Mwassa amewaagiza viongozi wa ngazi za Halmashauri na Wilaya kujipanga kufanya uhamasishaji na msako kwa wanafunzi wenye sifa walistahili kwenda shule waweze kwenda.
Katika hatua nyingine Mhe. Fatma Mwassa amesema kuna haja ya kuhamasisha wazazi kupitia kamati za shule kwa lengo la kuwapatia watoto chakula cha mchana wawapo shuleni ili kuongeza hali ya Ufaulu wa masomo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa