Picha ya hapo juu inaonyesha sehemu ya Tambiko ya Chifu wa Utengule
SEHEMU YA KWANZA.
Mabaki ya gari alilokuwa akitumia chifu Kiwanga
Ofisi ya utamaduni ilipata fursa ya kuzifikia kata sita ili kujifunza na kukusanya habari za kihistoria na kitalii za wilaya ya kilombero ambazo taarifa zake za awali ziliifikia ofisi kupitia watendaji kata.
Kata zilizotembelewa ni Utengule,Mlimba,Chisano,Chita Mchombe na Mbingu.Katika kata za Mlimba,Chita ,Mchombe na Mbingu walialikwa wadau wa Utamaduni wa kata za jirani ili kupata nafasi za kujadiliana juu ya maendeleo ya sekta ndani ya Halmashauri ya Kilombero.
KATA ZILIZOJITOKEZA
KATA YA UTENGULE
Kuna taarifa za Utawala wa Chifu Kiwanga ambao bado unaenziwa hadi hivi sasa.
Chifu aliyeonwa alijitambulisha kwa jina la Chifu Soliambingu wa pili.Chifu huyo aliupokea Uchifu kutoka kwa ChifuTowegale wa pili tangu 2008.
Chifu aliwabainisha machifu waliomtangulia kwa kufuatana kama ifuatavyo; Chifu Manga,Chifu Kihegula,Chifu Luvatu,Chifu Mgovano,Chifu Ndivale,Chifu Msavila,Chifu Mtengela,Chifu Kiwanga wa Kwanza ambaye Utawala wake Uliishia 1905,Chifu Kiwanga wa Pili ,Chifu Soliambibgu wa Kwanza,ChifuTowegale wa kwanza,Chifu Towegale wa pili na Mwisho Chifu Soliambingu ambaye anaendeleza Utawala huo hadi sasa kuanzia mwaka 2008.
ENEO LA MAKAZI YA CHIFU KIWANGA
Katika makao makuu ya Utawala wa chifu Kiwanga ambapo palijulikana kama IGOMBE yaani ikulu ya chifu yameonekana majengo kadhaa ambayo kwa sasa ni magofu nayo ni jengo la Mahakama ya Utawala wa kichifu ,Mabaki ya Gari alilotumia chifu,Mnara wa nyumba ya tambiko,shule,na nyumba ya Utawala yaani Ikulu.
Mabaki ya iliyokuwa ikulu ya chifu Kiwanga
Chifu Soliambingu wa pili alitueleza kuwa, enzi za Utawala wa chifu Towegale zilikuwa miaka ya 1920-1961,Chifu Towegale wa pili 1961-2008 na chifu Soliambingu wa pili 2008 hadi sasa.
Chifu alibainisha ngoma zilizokuwa maarufu enzi zao zilikuwa, Luheyo,Lipala,Liketo na Mdulange. Chifu alisema akipewa nguvu ya kufufua ngoma hizo yuko tayari kwani bado ana uwezo wa kuzifundisha.Nguvu aliyoisema ni pamoja na Gharama za Maleba,Ngoma,Vifaa vingine vya kukamilisha ngoma,gharama za mafunzo kwa vijana na wazee, uandaaji matamashana Recording.
Chifu aliongeza kuwa Katika enzi za utawala wake kulikuwa na bwawa maarufu lililojulikana kama Ngapemba ambapo wakati wote lilikuwa na maji mengi na kutoa samaki kwa wingi kukidhi jamii yao.Bwawa hilo kwa sasa limepoteza umaarufu wake kutokana na ukiukwaji wa baadhi ya miiko ya matumizi ya bwawa hilo
Chifu aliongeza kuwa usafiri maarufu wa machifu ulikuwa ni mitumbwi 3 ya usafiri wa majini na Gari la kifahari kwa ajili ya nchi kavu. Katika safari alieleza kuwa chifu alikuwa akisafiri na wake zake kati ya 60 na 70.
Mwisho chifu aliomba uhisani serikalini kwa ajili ya kukarabati majengo ya utawala huo ili kutunza historia ya utawala ingawaje kwa sasa hauna majukumu mazito kama enzi zake. Aidha aliomba uwepo utaratibu wa historia hiyo kufundishwa mashuleni hii ni pamoja na mila,desturi nzuri na ngoma za asili.
Je unataka kujua habari juu ya chura wanaozaa? Endelea kutembelea website yetu kwaajili ya sehemu ya pili ya maelezo haya.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa