Mhe. Jenista J. Mhagama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) @owm_tz amewaongoza Mawaziri, Manaibu mawaziri na Makatibu wakuu wa Wizara kufanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kuangalia athari ya Uharibifu wa Miundombinu ya reli, Barabara na makazi ya watu yaliyotokana na mafuriko yaliyoikumba kata ya Masagati na maeneo ya Jirani.
Aidha Mhe. Mhagama amewapa salamu za Upendo wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kutoka kwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuwapa pole kwa changamoto ya mafuriko na kuendelea kuwasisitizia wananchi wote waliojenga na kufanya shughuli kwenye mabonde wahame.
Mhe. Mhagama pia amemwelekeza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro kuhakikisha ndani ya Wiki ikayo anafanya mikutano ya Hadhara na wananchi wote ambao mradi wa Ujenzi ya Barabara ya lami kutoka Ifakara hadi Igima unapita kwenye maeneo yao na kuwaelezea hali ya utekelezaji wa Miradi huo pamoja na kumtambulisha Mkandarasi kwa wananchi.
Mhe. Judith Salvio Kapinga Naibu waziri wa Nishati amemwelekeza Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro kuhakikisha anasimamia suala la kuondoa hali ya ukatikaji kwa umeme katika Mkoa wa Morogoro pamoja na kurekebisha tatizo la Trasforma katika kijiji cha Matangini kata ya Mlimba.
Pia, Mhe. David Silinde @davidsilinde Naibu waziri wa kilimo amewajulisha wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kuwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan atasaini Mkataba kwa ajili ya kuleta mshauri mwelekezi atakayepitia Bonde lote la mto Kilombero kwa ajili ya skimu za Umwagiliaji pamoja na mabwawa makubwa ya kuhifadhi maji ili wananchi walime mwaka mzima.
Mhe. Jerry Sila @jerrysilaa Waziri wa Ardhi, nyumba na makazi amewaelekeza Maafisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba na kamishina wa Ardhi Mkoa wa Morogoro kuandaa taarifa ya matumizi bora ya ardhi katika kijiji cha Mlimba B kitongoji cha TAZARA pia Mhe. Silaa amewahidi wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kurudi kwa ajili ya kusikilia kero za Wananchi pamoja na Shamba la Rubada.
Mhe. Juma Aweso @jumaa_aweso Waziri wa Maji amemwelekeza katibu Mkuu wizara ya maji @wizarayamajitz kuleta Bilioni Moja katika kukamilisha mradi wa maji Mlimba.
@kyobyad @dc.kilombero
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa