• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MLIMBA DISTRICT COUNCIL
MLIMBA DISTRICT COUNCIL

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA

  • Mwanzo
  • kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/ Asili
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
      • Muonekano wa muundo
    • Idara/ Vitengo
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Miundombinu
      • Fedha na Biashara
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, Takwimu na ushirika
      • Mazingira na Usafi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Maji
      • Ardhi, Maliasili na Mazingira
      • Ufugaji na uvuvi
      • CHF iliyoboreshwa
      • Sheria
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Msingi
      • Sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za watumishi
    • Rasilimali watu
    • TEHAMA
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha, utawala na mipango
      • Elimu, Afya na maji
      • Uchumi, Ujenzi na mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Kumuona mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
      • PICHA ZA MIRADI YA MAPAMBANO DHINI YA UVICO

Mkuu wa wilaya ya kilombero awaonya viongozi wa Namwawala kuhusu usafi

Posted on: June 4th, 2018

Pichani: Mkuu wa wilaya ya Kilombero Ndugu James Ihunyo, akizungumza na wanakijiji wa kata ya Namwawala.

MKUU Wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo, amesema kuwa ndani ya wilaya hiyo kama kutatokea magonjwa ya kujitakia ya mlipuko, basi kiongozi Wa eneo husika lazima achukuliwe hatua.

Ihunyo ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati akizungumza na wananchi sambamba na kulitambulisha shirika jipya lisilokuwa la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Afya na usafi wa mazingira la HAPA, katika kata ya Namwawala wilayani humo.

Mkuu huyo Wa Wilaya amesema, ni aibu kwa kiongozi katika eneo lake kutokea magonjwa ya milipuko kama kipindupindu ama kuhara na kusema kuwa, magonjwa hayo ni ya kujitakia na yanazuilika pale kiongozi atakapotimiza wajibu wake katika usafi.

"Kusikia eti kijiji ama kata kuna mlipuko Wa kipindupindu ni aibu, kwani ugonjwa huo unazuilika kwa kuweka mazingira safi ikiwemo kuwa na choo bora, sasa ukisikia mlipuko umetokea basi ujue kiongozi huyo hafai, kwani hakuwasimamia wananchi wake katika suala la  usafi Wa mazingira " alisema.

Amewaagiza viongozi kuanzia ngazi ya vitongoji kufanya ukaguzi Wa Mara kwa Mara, kuhusu usafi katika kaya zinazowazunguka ikiwemo vyoo bora na familia yeyote isiyo na choo, ikamatwe na kupelekwa katika vyombo vya Sheria.

"Mlipuko Wa magonjwa ya kuhara na kipindupindu yanatokana na uchafu unaotokana na kula kinyesi, nanyi Sheria ndogo mnazo kwa nini hamzitumii watu kuwakamata ama kuzuia kujisaidia ovyo bila kuwa na choo?" Alihoji.

Amesema hapendi kuona hali iliyopo hivi sasa kwa asilimia 80 ya wagonjwa wanaoenda hospitali, kuonekana wanaugua magonjwa yanayotokana na tatizo la uchafu, ikiwemo kipindupindu na kuhara.

Mkuu huyo Wa Wilaya amesema, katika kuhakikisha hayatokei magonjwa ya kujitakia ya mlipuko katika Wilaya hiyo, amewaagiza watendaji kuanzia ngazi ya vijiji na kata, kuandaa mashindano ya usafi wa mazingira na choo bora na washindi kupewa zawadi mbalimbali na hiyo itahamasisha kila Mwananchi ndani ya Wilaya hiyo, kuwa na choo bora na kuwa na mazingira bora.

Naye Afisa Afya katika halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mbonja Kasembwa alisema kuwa, halmashauri kwa kushirikiana na shirika la HAPA wamefanikiwa kutembelea Wilaya nzima, na kuhamasisha suala LA mazingira na ujenzi Wa vyoo bora na asilimia 80 ya wananchi wake kwa sasa wana vyoo bora.

Katika hatua nyingine, Meneja mradi Wa shirika la HAPA Baraka Mwakubali amesema, mradi huo toka uanze mwaka Jana kwa kushirikiana na halmashauri umekuwa na mafanikio makubwa, ila ametoa ushauri kwa vijiji ambavyo mazingira yake ni safi, na kaya kuwa na choo vianze mchakato Wa kuhamasisha kaya zijenge vyoo bora vya kisasa.

Mwakubali amesema kwa vijiji ambavyo kaya zake hazina vyoo, viendelee kuhamasisha ujenzi Wa vyoo pamoja na kutumia Sheria ndogondogo za vijiji, katika kuhakikisha kaya zinajenga vyoo na pia viongozi junamosi ya mwisho wa mwezi, wakague hali ya usafi Wa mazingira na ujenzi Wa vyoo, pamoja na uwepo Wa vifaa vya kunawia mikono vyenye Maji na Sabuni.

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI NA MWENDESHAJI WA VIFAA VYA BAYOMETRIKI February 13, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA KUSIMAMIA UCHAGUZI MKUU 2025 July 03, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA DEREVA NA MWENDESHA OFISI MLIMBA DC July 01, 2025
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA MWEZI DESEMBA 2024 January 07, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MLIMBA YAPANGIWA WAAJIRIWA WAPYA 73

    July 04, 2025
  • MKURUGENZI JAMARY AWAPOKEA MADAKTARI BINGWA WA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    June 10, 2025
  • MHE. WAZIRI WA MAMBO YA NJE KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MLIMBA DC

    June 04, 2025
  • MLIMBA DC YAPOKEA VITABU 13,607 KWA AJILI YA SHULE ZAKE ZA SEKONDARI

    May 30, 2025
  • Angalia zote

Video

Kupata Madarakani au cheo hakukufanyi kujua kila kitu. Maneno ya hekima kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu Mhe. Mhe. Dkt Doto Biteko
video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Fomu ya maombi ya ruhusa
  • Fomu ya utambulisho benki
  • Fomu ya Kuhuisha Uanachama CHF iliyoboreshwa
  • Wasifu wa Wilaya
  • Muundo wa Halmashauri
  • Eneo la Kijiografia
  • Fursa za Uwekezaji Kilombero

Viunganishi linganifu

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Idara kuu ya Takwimu (NBS)
  • TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

kitafutio cha watembeleaji wa duniani

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Mngeta Kijiji cha Itongoa

    Anuani: P.O.BOX 263

    Simu: 023 293 1523

    Mobile: 0232931523

    Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa