CHF iliyoboreshwa ni kadi maalumu itakayomuwezesha mwananchi kuweza kutibiwa katika hospitali yoyote ya serikali na binafsi kwa gharama nafuu kwa wananchi wake. Gharama ya kadi hii ni shilingi alfu thelathini tu, ambapo baada ya kutoa pesa hiyo utapewa kadi yako moj na ya wategemezi wako watano ambao wote mtatibiwa bure kwa muda wa mwaka mmoja kabla hujalazimika kulipia tena gharama hiyo kwaajili ya kupata huduma hiyo kwa mwaka mwingine.
huduma hii ni mpango madhubuti wa wakazi wa kilombero ambapo umewekwa ili kupunguza vifo vya mara kwa mara kwa kukosa pesa za matibabu ambayo ni gharama sana, ambapo kadi hii imeonekana kuwa mkombozi mkubwa kwa maendeleo ya wana kilombero.
kwa maelezo zaidi tafadhali ukiwa kama mkazi wa Halmashauri ya kilombero tembelea hospitali yoyote iliyo karibu nawe ili uweze kusaidiwa
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa