Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba limeketi na kupitisha taarifa za utekelezaji na miradi ya maendeleo kwa kipindi Cha robo ya tatu 2023/2024. Pamoja na mambo mengine ya utekelezaji wa Halmashauri.
Aidha Baraza la leo limeshuhudia Diwani Mteule wa kata ya Kamwene Mhe. Zugumbwa G. Mbaruku akiapishwa na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mngeta na kuanza rasmi majukumu yake baada kuchaguliwa kufuatia kifo Cha aliyekuwa Diwani wa kata hiyo ambapo Baraza limempokea na kumpongeza Diwani huyo.
Baraza la Madiwani limempongeza na kumshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwajali na kuwapatia mahitaji wananchi waliopata maafa kutokana na mafuriko hususani katika kata ya Masagati na Utengule. Pamoja na mambo mengine, Baraza limefanya mabadiliko ya ushuru wa Mchele kutoka bei ya shilingi 4500 Hadi 3000 kwa kueleza kuwa sasa bei ya Mchele imeshuka tofauti na hapo awali ilipokuwa juu.
Menejimenti ilipokea maelekezo ya Baraza la madiwani na kuahidi kuyafanyia kazi kulingana na Sheria Ndogo za Halmashauri pamoja na Sheria ya mapato ambayo inataka ushuru utozwe sio zaidi ya asilimia tatu ya Bei ya soko.
Kwa upande Mwingine, Baraza limeelekeza Menejimenti kuhakikisha wanakamilisha kazi ya kuzungumza na wawekezaji juu ya mashamba ya Halmashauri yaliyoko kata ya Masagati na Utengule ili kuwekeza na Halmashauri ipate mapato.
Mhe. Innocent Mwangasa Mwenyekiti wa Halmashauri ameelekeza Mpango wa Halmashauri kuendeleza vipaji vya Wananchi wa Halmashauri kwa kuhakikisha kila Diwani ahakikishe Michezo, Sanaa na Utamaduni inafanyika kwa kila kata na vile vipaji vinavyofanya vizuri viwekewe Mpango mkakati wa kuviendeleza katika tasnia zao ili kuwezesha Vijana kuweza kujiajiri na kuajiriwa.
Mhe. Makao Diwani kata ya Masagati ameendelea kutoa shukrani za dhati kwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapatia mahitaji ya Chakula wananchi wa kata ya Masagati waliokumbwa na a-dhia ya mafuriko, pia amemshukuru Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Godwin Kunambi @godwin_kunambi Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Mhe. Adam Kighoma Malima Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dunstan Kyobya @kyobyad @dc.kilombero Mkuu wa Wilaya Kilombero pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali.
Pia, Mkuu wa Kituo cha Polisi Mngeta Afande Dotto amehakikisha hali ya Usalama inaendelea vizuri katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba na kuwasisitiza zaidi wananchi wa kata ya Mngeta na Mchombe kufata sheria na taratibu na kwa kipindi hiki kumezuka tabia hatarifu ya Ubakaji kwa maeneo hayo na kuhakikisha Askari Polisi wapo Imara kuhakikisha vitendo vyote viovu vinatokomezwa.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa