BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA LAPITISHA BAJETI YA KIASI CHA SHILINGI 33,568,691,564.00.
Baraza la madiwani limepitisha bajeti ya kiasi cha Shilingi 33,568,691,564.00 kwa vyanzo vingine kutoka Serikali Kuu ambayo mishahara ni bilioni 18,391,888,904.00 na ruzuku ya OC na miradi ya Maendeleo. Bajeti hiyo imezingatia vyanzo vikuu vitano vinavyochangia makusanyo kwa kiasi kikubwa katika Halmashauri ambavyo ni :-
Mchele, Ushuru wa huduma, mazao ya misitu, ufuta na sehemu za huduma vyanzo vyote hivi vinachangia kwa asilimia 78 na vyanzo vingine vinachangia kwa asilimia 22.
Kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri inakadiria kukusanya jumla ya Kiasi cha Shilingi 6,141,886,750 kutoka vyanzo vyake vya ndani ambapo mapato halisi kiasi cha Shilingi 4,833,800,750.00 na Mapato fungwa kiasi cha Shilingi 1,308,086,000.00.
Halmashauri imepanga kutekeleza miradi 17 kwa mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kutoka Divisheni na Vitengo mbalimbali. Miradi ya kimkakati inayotarajiwa kutekelezwa inagharama ya kiasi cha Shilingi 15,442,010,853.00 miradi hiyo ni ujenzi wa skimu ya Umwagiliaji bonde la Kisegese na uanzishaji wa kiwanda cha kuchakata mpunga Kisegese.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa