• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MLIMBA DISTRICT COUNCIL
MLIMBA DISTRICT COUNCIL

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA

  • Mwanzo
  • kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/ Asili
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
      • Muonekano wa muundo
    • Idara/ Vitengo
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Miundombinu
      • Fedha na Biashara
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, Takwimu na ushirika
      • Mazingira na Usafi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Maji
      • Ardhi, Maliasili na Mazingira
      • Ufugaji na uvuvi
      • CHF iliyoboreshwa
      • Sheria
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Msingi
      • Sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za watumishi
    • Rasilimali watu
    • TEHAMA
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha, utawala na mipango
      • Elimu, Afya na maji
      • Uchumi, Ujenzi na mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Kumuona mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
      • PICHA ZA MIRADI YA MAPAMBANO DHINI YA UVICO

BARAZA LA MADIWANI NA USTAWI WA HALMASHAURI

Posted on: January 20th, 2025

TAARIFA KWA UMMA

Ijumaa ya tarehe 17.01.2025, Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Mlimba liliketi kujadili na kufanya maamuzi muhimu kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji na maendeleo ya halamshauri hiyo. Baadhi ya maamuzi makubwa yaliyo fikiwa na Baraza hilo ni kama ifuatavyo:

1. Uteuzi na Kusitishwa kwa Ajira za Watumishi: Baraza limeamua kusitisha ajira kwa watumishi wawili watoro kazini kwa muda mrefu kinyume cha taratibu. Aidha, Baraza limeidhinisha uteuzi wa watumishi wawili waliokuwa wanakaimu vitengo kuwa wakuu wa vitengo hivyo. Pia limeidhinisha uteuzi wa mtumishi mmoja kuwa mkuu wa idara ya rasilimali watu.

2. Masuala ya Kisheria: Baraza pia limefanya uamuzi wa kufuta madeni kwa wadaiwa wanne ambao walishinda kesi dhidi ya halmashauri.

Maagizo ya mkuu wa Wilaya:

Katika ufunguzi wa kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, mhe. Wakili Dunstan Kyobya alitoa maagizo kadhaa kwa madiwani na Halmashauri ya Mlimba kwa ujumla, ikiwemo:

1. Utekelezaji wa Miradi na Ushirikishwaji wa Wananchi: Mkuu wa Wilaya amelipongeza Baraza kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo, na pia ameipongeza halmashauri kwa kuwashirikisha wananchi katika utekelezaji wa miradi hiyo. “Miradi ipo kwenye kila kata, hongereni sana Mlimba”alieleza.

2. Ukusanyaji wa Mapato: Amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri, mhe. Innocent Mwangasa na Baraza lote kwa kuwa kinara nchini mpaka sasa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani. “Kwa sasa ninyi ndio mnaongoza nchi nzima na kimkoa, mapato yenu ni wastani wa 95% tunatumai mpaka mwezi ujao mtafika 100%, hongereni sana” alisema.

3. Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania: Mkuu wa Wilaya amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika sekta za elimu na afya, hatua inayolenga kupunguza na kutokomeza kabisa ujinga na maradhi, mambo ambayo ni adui wa maendeleo katika Taifa.

4. Elimu kwa Watoto: Ameagiza kuwa watoto wote wenye umri wa kuanza darasa la awali, darasa la kwanza na walio chaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, waende shule bila kujali kama wanazo sare au la, ili kuhakikisha kuwa elimu inapatikana kwa wote.

5. Usalama, Lishe, Utoro na Uhifadhi wa Mazingira: Ameagiza kuwa masuala ya usalama, Lishe, utoro, uhifadhi na utunzaji wa mazingira yawe agenda za kudumu kwenye vikao na mikutano ya madiwani katika maeneo yao ya utawala.

6. Vitongoji na Daftari la Wakaazi: Ameagiza vitongoji vyote kuwa na daftari la wakaazi ili kubaini wageni na kutoa taarifa zao kwenye mamlaka husika, kufanya hivi kutaimarisha ulinzi na usalama wa raia ndani ya halmashauri.

7. Kupanda Miti: Mkuu wa Wilaya ameagiza halmashauri kupanda miti ya Kokoa, Chikichi, Korosho, Parachichi na zao la Pamba kwa wingi kadiri iwezekanavyo ili kufikia lengo la Wilaya la kupanda miti milioni tatu kwa mwaka huu 2025.

8. Mikopo ya Asilimia 10 kwa Vikundi: Ameagiza utoaji wa mikopo kwa vikundi vyote vinavyo kidhi vigezo, na vikundi vyenye madeni viendelee kuchukuliwa hatua ili virejeshe na wengine wakopeshwe. “Mpaka sasa halmashauri hii ndio ambayo imetoa fedha nyingi za mikopo ya asilimia 10 kuliko halmashauri zingine za mkoa wa Morogoro” alipongeza.

9. Umeme Katika Vitongoji: Amewataka madiwani kutoa taarifa kuhusu vitongoji ambavyo bado havijawashiwa umeme kwenye awamu hii ya tatu ya umeme wa REA katika Halmashauri ya Mlimba, endapo vipo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na madiwani wa kata zote 16, viongozi wa wananchi ngazi ya kata, vijiji na vitongoji, na watumishi wa halmashauri. Baraza lilijadili kwa kina masuala mbalimbali ya maendeleo ya Halmashauri yaliyofanyika katika robo ya pili (Oktoba-Desemba), ya mwaka huu wa fedha 2024/2025 na kuhimiza ushirikiano zaidi kati ya halmashauri na wananchi ili kuendelea kufanikisha malengo ya maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya Mlimba.

MWISHO

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Tarehe 20.01.2025.


Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI NA MWENDESHAJI WA VIFAA VYA BAYOMETRIKI February 13, 2025
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA MWEZI DESEMBA 2024 January 07, 2025
  • KIUNGANISHI (LINK) YA MATOKEO YA MTIHANI WA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI MWAKA 2024 January 05, 2025
  • KIUNGANISHI (LINK) CHA MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA UPIMAJI WA DARASA LA NNE MWAKA 2024 January 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI JAMARY AWAPOKEA MADAKTARI BINGWA WA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    June 10, 2025
  • MHE. WAZIRI WA MAMBO YA NJE KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MLIMBA DC

    June 04, 2025
  • MLIMBA DC YAPOKEA VITABU 13,607 KWA AJILI YA SHULE ZAKE ZA SEKONDARI

    May 30, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAPOKEZI YA VIFAA VYA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Kupata Madarakani au cheo hakukufanyi kujua kila kitu. Maneno ya hekima kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu Mhe. Mhe. Dkt Doto Biteko
video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Fomu ya maombi ya ruhusa
  • Fomu ya utambulisho benki
  • Fomu ya Kuhuisha Uanachama CHF iliyoboreshwa
  • Wasifu wa Wilaya
  • Muundo wa Halmashauri
  • Eneo la Kijiografia
  • Fursa za Uwekezaji Kilombero

Viunganishi linganifu

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Idara kuu ya Takwimu (NBS)
  • TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

kitafutio cha watembeleaji wa duniani

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Mngeta Kijiji cha Itongoa

    Anuani: P.O.BOX 263

    Simu: 023 293 1523

    Mobile: 0232931523

    Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa