Pichani juu: mkuu wa wilaya Ndg James Ihunyo (aliyemshika mtoto) akiwa na wakaazi mbalimbali wa eneo la Chita waliojitokeza katika Tamasha la TAYOA, mapema jana.
Shirika lisilo la kiserikali la TAYOA mapema mwishoni mwa wiki hii, limefanya Tamasha kubwa sana la kihistoria, katika Halmashauri ya wilaya ya Kilombero katika kata ya Chita, kwa lengo la kuwaleta karibu wasichana balehe na kuwafunza kuhusu namna ya kujielewa kwenye maisha yao.
Tamasha hilo lililoambatana na upimaji wa virusi vya UKIMWI na michezo mbalimbali ikiwamo kukimbiza kuku kwa wasichana, kuvuta kamba kwa wasichana, kukimbia na magunia kwa wasichana na mpira wa miguu uliowahusisha wasichana na wavulana lilifana sana na kuteka hisia za wakazi wengi sana wa eneo hilo.
Katika kuonyesha kuwa tamasha hilo limefanikiwa, walijitokeza vijana wengi sana kutoka maeneo ya jirani na hata vitongoji vya mbali huko, lengo likiwa ni kupata ujumbe, kungalia afya zao bure na kuburudika kutokana nay ale ambayo yalikuwa yameandaliwa na asasi hii kwa kushirikiana na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Akizungumza katika Bonanza hilo mkuu wa wilaya ya Kilombero ndugu James Ihunyo, ambae ndie aliyekuwa mgeni rasmi, amesema kuwa, anawapongeza sana hawa TAYOA kwa kuamua kuja kulifanyia tamasha hilo huko Chita, kwani itasaidia sana kuwapa fursa za watu kuweza kujua afya zao, na kuwapa nafasi ya kuamua juu ya maisha yao.
Akizungumzia tamasha hilo, mratibu wa UKIMWI wa wilaya ya Kilombero bi Hawa Mdoka amesema kuwa, vijana wengi wamekuwa katika hatari ya kupata maambukizi pasipo kuwa na utambuzi wowote ama kudharau tu, hivyo basi kampani hii ipo mahsusi kwaajili ya kuwazindua vijana waondokane na matatizo hayo ambayo ni janga kubwa sana la kitaifa.
Nae mratibu wa Bonanza hilo ndugu Adam ameongeza kuwa, kuna umuhimu mkubwa sana wa watoto wa kike na vijana kwa ujumla kujitambua kuwa wao ni kina nani hususan pale wanapokuwa wamefikia umri wa ukuwbwa, hivyo ni bora kila kitu kikawa sawa mapema kwenye suala zima la kujitambua, kabla mambo hayajawa mabaya kwa vijana hao.
Mwisho kabisa akitoa zawadi na kutambulisha baadhi ya vitu katika asasi hiyo, mkurugenzi wa asasi hiyo ya Vijana ya TAYOA ndugu Peter Msika alisema kuwa, kutokana na ushirikiano waliouonyesha wana Kilombero kwa kujitokeza kwa wingi na kufanya upimaji kwa zaidi ya aislimia 85 ya wakazi wa eneo hilo kulingana na takwimu zake, ameamua kuleta tena tamasha hilo mnamo mwezi wa kumi na moja huku akiongeza zawadi na burudani zaidi kwa wakazi wa eneo hilo
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa