Pichani juu: Injinia Stephano Kaliwa (aliyenyanyua mkono juu) akimuelekeza jambo Mkuu wa wilaya ya Kilombero Ndg Ismail Mlawa (Mwenye Tai Nyekundu) Katika eneo la ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kilombero Ndg Ismail Mlawa, amempongeza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa, kwa juhudi kubwa alizozifanya kuhakikisha kuwa ujenzi wa Hospitali ya wilaya unafikia kiwango kilichofika kwa sasa Pamoja na changamoto za mazingira ya eneo hilo la ujenzi.
Akizungumza katika siku ya tatu ya ziara yake katika wilaya yake, mapema jana, Ndg Mlawa amesema kuwa Pamoja na kwamba eneo hilo la ujenzi lipo juu ya milima, lakini Halmashauri imefanya jitihada za kutosha kutafuta mtambo wa kuukata mlima huo na kuweka msawazo (level) ili kuweza kurahisisha shughuli za ujenzi huo kwa mujibu wa kasi ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli.
Katika Hatua nyingine amemsisitiza mkandarasi kuhakikisha kuwa, anamaliza ujenzi huo kwa muda uliopangwa, na kama ikitokea uzembe wowote ule serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria, kwani hiyo ndio kazi inayotakiwa kwa awamu hii ya tano.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Mlimba amesema kuwa, Pamoja na kwamba Halmashauri imehamishiwa Mngeta mapema mwezi wa kumi na moja mwaka jana lakini watahakikisha wanakamilisha miradi yote waliyojipangia kuitekelezaikiwa ni Pamoja na ujenzi huo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na kwa muda muafaka.
‘’ Pamoja na kwamba tumefika hapa mngeta mwaaka jana mwezi wa kumi na moja, hiyo haiwezi kutuzuia kuhakikisha kuwa tunatekeleza miradi yote tuliyojipangia ikiwamo ujenzi huo wa Hospitali ya wilaya utakaokwenda sambamba na ujenzi wa ofisi mpya ya Halmashauri yetu.’’ Alisema kaliwa.
Habari Picha.
Harakati mbalimbali za ukaguzi huo
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa