pichani: diwani Songo Daniel akionyesha moja ya fomu aliyoisaini kwaajili ya kuunga mkono juhudi za kuishawishi serikali kuongeza muda wa wasichana kuolewa kisheria.
Diwani Songo Daniel wa kata ya kisawasawa katika halmashauri ya wilaya ya Kilombero, amesema kuwa ili kusitisha ndoa za utotoni, anawaomba wadau wote na watanzania kwa ujumla kumuunga mkono kusaini kwenye fomu zake kwa lengo la kuishawishi serikali kufanya marekebisho ya umri upasao, kwa motto wa kike kuolewa kutoka miaka 14 ya sasa kisheria mpaka miaka 18 ambapo motto angalau atakuwa amekwishajitambua na anaweza kuamua kile anachokitaka na kile asichokitaka.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Mhe. Songo amesema kuwa kwa upande wa kilombero, kuna matatizo makubwa sana ya watoto wa kike kuolewa pindi tu wanapomaliza shule na hii hupelekea watoto wengi sana kufa kutokana na kujifungua katika umri mdogo kabla ya kupevuka.
Akitoa mfano mhe. Songo alisema kuwa ikiwa utapata nafasi ya kutembelea kwenye hospitali kadhaa za hapa Kilombero unaweza kukuta asilimia karibu 60 ya wakinamama wanaohudhuria kliniki ni watoto wadogo kabisa walio chini ya umri wa miaka 18, jambo ambalo ni matatizo makubwa sana kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu.
Akisisitiza alisema kuwa, atahitaji kugawa fomu kwani anazo nyingi mno kutoka shirika la kimataifa la plan international kwaajili ya kushirikiana pamoja kuishawishi serikali kuifutilia mbali sheria hii ili watoto wa kike waweze kurudi mashuleni na kuhakikisha kuwa wanatimiza ndoto zao walizojiwekea katika maisha yao.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa