Rais mteule wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mapema leo ameapishwa na Jaji mkuu wa Tanzania, katika viwanja vya jamhuri Dodoma kuw Rais wa nchi hii kwa mara ya pili katika awamu yake
Dkt. Magufuli amewashukuru sana wakaazi wa Dodoma kwa ushirikiano mkubwa sana alioupata kutoka kwao na watanzania kwa ujumla.
Amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kimepata ushindi mkubwa kutokana na baraka za wana Dodoma kwa sababu uzinduzi na kilele cha kampeni za uchaguzi mkuu zilifanyika Jijini Dodoma. “Yote tuliyoahidi tutayashughulikia ikiwemo ujenzi wa barabara ya mzunguko, sababu msongamano umeanza kuonekana Dodoma” aliongeza Rais huyo.
Akitoa salamu kwa niaba ya wananchi wa Jamhuri ya Comoro, Rais wa nchi hiyo, Azali Assoumani alimuomba Mungu kumsaidia sana Rais, Dkt. Magufuli kutekeleza kazi aliyopewa na watanzania kwa ufanisi.
“Nachukua nafasi hii kuwapongeza wananchi wa Tanzania kukamilisha salama mchakato wa uchaguzi, nawashukuru kwa uwepo wao hapa. pia ninamuomba mungu kumsaidia Dkt Magufuli kutekeleza kazi aliyopewa na watanzania” alisema Rais Assoumani.
Nae, Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa alisema “naleta salamu nyingi kutoka kwa wananchi wa Zimbabwe. Tunamshukuru Rais, Dkt. Magufuli alifanya ziara nchini Zimbabwe. Na wakati wa ukame mkali, Rais Dkt. Magufuli alitupatia msaada wa mahindi kwa Wazimbabwe. Huyu ni kiongozi mzalendo katika ukanda huu”.
Wakati huohuo, Mwanazuoni na Mhadhiri wa Sheria kutoka Kenya, Prof. Patrick Loch Otieno Lumumba kupitia televisheni ya TBC amempongeza Rais, Dkt. Magufuli na CCM kwa ushindi mkubwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Prof. Lumumba ametoa tahadhari kuwa makini na wafadhili wavurugaji nchi za kiafrika. “Katika nchi za kiafrika, tuwe wepesi kujiepusha na wafadhili wenye lengo la kuvuruga nchi za Afrika. Tatizo la nchi za Afrika ni kutotofautisha upinzani na ubabaishaji. Tuhakikishe tunaendesha siasa ambazo zinalinda usalama wetu” amesema Prof. Lumumba kwa msisitizo.
Habari katika picha
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa