Halmashauri ya wilaya ya Kilombero imekokotoa upya viwango vya ushuru vya mpunga kutoka shilingi 2500 hadi kufikia shilingi 1700 kwa gunia la debe saba.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Dennis Londo amesema maamuzi hayo yametokana kufuatia azimio la kikao cha kamati ya fedha,utawala na mipango kilichofanyika mwishoni mwa mwaka 2017 mjini Ifakara wilayani humo.
Londo amesema kwa kuzingatia wastani wa bei ya soko la mpunga na mchele,na kwa kuzingatia matakwa ya sharia ya vipimo,ni kwamba gunia la mpunga liwe na ujazo wa debe saba za mpunga.
Amesema pamoja na matakwa ya sharia ya fedha ya umma,marekebisho yam waka 2017 halmashauri imekokotoa upya viwango hivyo vya ushuru vya mpunga na mchele ambapo sasa bei ya ushuru wa mpunga utakuwa shilingi 1700 na ushuru wa mchele utakuwa shilingi 3000 kwa kilo 100.
Mkurugenzi huyo amesema baada ya agizo hilo wataalamu wa halmashauri wamerekebisha viwango hivyo vya ushuru kwenye mashine za kutolea risiti za kieletroniki na tokea Disemba 18 mwaka 2017 viwango vipya vimeanza kutumika.
Hata hivyo mkurugenzi huyo amewahamasisha wananchi kudai risiti za kieletroniki na kuzingatia matakwa ya sheria ya vipimo kuhusu ujazo wa gunia la mpunga na halmashauri itatoza faini kwa mwenye gari na mwenye mali kutokana na ukiukwaji wowote wa sheria hizo.
Aidha inasisitizwa kwamba halmashauri itaendelea kutowatoza ushuru wakulima wote waliotambuliwa kwa kupewa vibali vya utambuzi na wanaosafirisha mazao yasiyozidi tani moja na halmashauri inaomba ushirikiano wa kila mwananchi mwenye nia njema ili kwa pamoja kuijenga Kilombero.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa