Pichani juu: mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero ndg David Ligazio (kulia) pamoja na makamu mwenyekiti Hilda Mahimbali (kushoto) wakifuatilia hoja za wajumbe kwenye baraza la madiwani
BARAZA la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kilombero limetekeleza agizo la serikali na kuamua kata ya Mchombe tarafa ya Mngeta kuwa Makao makuu yake mapya ya halmashauri.
Tamko hilo limetolewa jana katika kikao cha dharura cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini Ifakara na kusema kuwa kuanzia sasa Makao yao makuu yatakuwa Mngeta hivyo shughuli zote za kiofisi zitahamia katika eneo hilo.
Ikumbukwe kuwa Oktoba 7 mwaka huu kupitia Waziri Wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na serikali za mitaa Seleman Jafo alizitaka halmashauri 31 ambazo ofisi zake zipo nje ya maeneo yao ya Utawala kuhamishia ofisi hizo katika maeneo yao ya Utawala.
Katika taarifa hiyo Waziri Jafo aliziagiza halmashauri hizo kwenda maeneo yao ndani ya siku 30 na agizo hilo lilianza kutekelezwa kuanzia Agosti 7 mwaka huu.
Katika utekelezaji huo halmashauri ya Wilaya ya Kilombero ni moja ya halmashauri hizo na hivyo kuamua kutekeleza agizo la serikali katika utekelezaji.
Mwenyekiti Wa halmashauri hoyo David Ligazio alisema kufuatia maagizo hayo kuanzia Leo Mji Mkuu Wa halmashauri hiyo utakwenda Mngeta na kuwataka watendaji na watumishi kutekeleza agizo la baraza.
Ligazio alisema ameiomba serikali kuwapatia majengo ya iliyokuwa ofisi ya ushirika baina ya Korea na Tanzania(KOTAKO) ili kuwa ofisi za muda za halmashauri hiyo.
Ligazio alisema kuanzia sasa vikao vyote vya halmashauri vitafanyikihamie ta na kuagiza menejimenti kufanikisha suala hilo.
Aidha Ligazio amesema Mali zote za halmashauri hiyo ambazo zitabaki katika halmashauri ya Mji Wa Ifakara inabidi ziendelee kutambuliwa japo zipo nje ya halmashauri hiyo.
Awali mkurugenzi Mtendaji Wa halmashauri hiyo Mhandisi Stephano Kaliwa alisema timu ya menejimenti ilipendekeza Makao makuu ya halmashauri ihamie kijiji cha Sagamaganga kata ya Signal kwa sababu ya kijiografia kijiji kipo eneo zuri kistratejia kwa kuwahudumia wananchi Wa majimbo yote mawili ya Mlimba na Kilombero.
Mhandisi Kaliwa alisema kijiji cha Sagamaganga kuna Kituo cha upashanaji habari kilicho chini ya ofisi ya Kilimo na jengo linafaa kuwa ofisi za muda za mkurugenzi pamoja na wakuu Wa idara na pia pana eneo Kubwa la ekari 9.
Hata hivyo kikao cha kamati ya Fedha na mipango kilichoketi Oktoba 15 wajumbe walipendekeza Makao makuu yahamie tarafa ya Mngeta kata ya Mchombe kwa sababu eneo la tarafa lina watu wengi kwa kuwa kuna kata 16 tofauti na upande Wa Kidatu una Kata 10 na pia eneo hilo litawezesha watendaji kuwa karibu na wananchi zaidi.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa