SERIKALI kuu imeipatia kiasi cha shilingi milioni 700 halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kwa ajili ya kuboresha vituo vya Afya na kununulia vifaa tiba.
Mwenyekiti Wa halmashauri hiyo David Ligazio aliyasema hayo katika kikao cha baraza LA madiwani Wa halmashauri hiyo kilichofanyika jana mjini Ifakara.
Ligazio amesema serikali ya awamu ya tano inaendelea kutoa huduma nzuri kwa wananchi katika halmashauri hiyo na moja ya jukumu kubwa ni kuboresha huduma za Afya kwa wananchi wake.
Amesema katika Fedha hizo shilingi milioni 500 zimetolewa kwa ajili ya kuboresha vituo vya Afya na kiasi cha shilingi milioni 200 zimeelekezwa katika upatikanaji Wa vifaa tiba.
Mwenyekiti huyo amesema Fedha hizo zimetolewa mwaka huu na hata mwaka Jana walipewa Fedha ambazo zilipelekwa kuboreshwa katika kituo cha Afya cha Mlimba ila mwaka huu watapanga wamepeleke kwenye Kituo kipi hapo baadae.
Amesema wamepewa wiki Mbili ili kupata utekelezaji Wa Fedha hizo na watatumia mfumo Wa "force account" ili kutumia Fedha hizo na ameahidi kuwa matumizi yake yatakwenda sawia na maelekezo toka serikalini.
Ligazio amebainisha kuwa Fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 700 zipo nje ya zile Fedha zinazopelekwa kila baada ya miezi mitatu katika vituo vya Afya na kusema kuwa kwa sasa halmashauri ina vituo vya Afya vinne ambavyo ni Mlimba,Mngeta,Mang'ula na Mgudeni.
Katika hatua nyingine baraza hilo limeazimia kumtimua kazi Ramadhani Kazimoto ambaye alikuwa Dereva Wa halmashauri hiyo baada ya kubainika kuwa alitumia vyeti feki wakati Wa ajira yake na hiyo imetokana na zoezi lililoendeshwa na serikali kuu hivi karibuni.
Pia baraza hilo limeazimia kuwa Salum Sadala ambaye ni Afisa Mtendaji aendelee na majukumu yake baada ya kupatikana na upotevu Wa shilingi milioni 4 Fedha za serikali na hii imetokana na halmashauri kuwa na upungufu Wa watendaji ila ametakiwa kulipa Fedha alizochukua.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa