pichani juu mkurugeni mtendaji Ndg Dennis Londo (Aliyesimama mwenye fulana nyeusi) akizungumza na wafanyakazi mara baada ya usafi wa kila mwisho wa mwezi.
Katika kuonyesha kuwa wanatekeleza maagizo ya mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muu ngano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, halmashauri ya wilaya ya Kilombero imeendelea na utaratibu wake wa kufanya usafi kil inapofika jumamosi ya mwisho ya mwezi.
Hali hiyo imejitokeza siku ya jumamosi ya mwisho wa wiki iliyopita, ambapo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kilombero ndugu Dennis Londo aliwaongoza wafanyakazi wa halmashauri hiyo kufanya usafi kwenye maeneo yote yanyozunguka ofisi zao.
Aidha aliwaambia wafanyakazi hao katika hafla ndogo ya chai mara baada ya kukamilika kwa usafi huo kuwa, suala la usafi ni muhimu sana sio tu kwasababu tunafuata taratibu za kiserikali lakini pia ni muhimu kwa afya zetu kwa kuushughulisha miili yetu lakini hata kwa kuweka tu mazingira yanayotuzunguka katika hali ya usafi.
Mwisho kabisa aliwashukuru sana waislamu wote, ambao walijitoa kwa moyo mkunjufu kuja kufanya usafi huo na kusema kuwa, anawaombea kwa mungu swaumu zao ziwe zenye kukubaliwa huku akisisitiza wale wote ambao walitakiwa wafunge na hawakufunga basi wakati mwingine waweze kupata nafasi ya kufunga.
zifuatazo ni picha mbalimbali zikionyesha wafanyakazi hao wakishiriki kwenye usafi huo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa