pichani juu mheshimiwa Rais John Magufuli, akizindua Daraja la mto Kilombero.
Rais John Pombe Magufuli amezindua daraja la mto Kilombero ambalo kwa sasa linaitwa daraja la Magufuli
Akitangaza jina hilo siku ya jumamosi tarehe 5/5/2018 wakati Rais akizindua, waziri wa Ujenzi,uchukuzi na mawasiliano, profesa Makame Mbarawa amesema ametoa jina hilo kutokana na juhudi alizozifanya Rais Magufuli wakati akiwa waziri wa ujenzi.
‘’Mheshimiwa Rais kwa mamlaka niliyopewa natangaza rasmi daraja hili litaitwa Magufuli, hii ni kutokana na juhudi kubwa uliyoiweka katika kufanikisha ujenzi wa daraja hili,’’ amesema.
Aidha daraja hilo lenye urefu wa zaidi ya mita 300, linaunganisha wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero, kitu kitakachoweza kurahisisha mawasiliano kwa urahisi sana ukilinganisha na kipindi cha awali ambapo eneo hilo lilikuwa ni changamoto kubwa sana, hususani kwenye suala zima la kusafirisha mazao kutoka pembezoni.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa