Pichani juu: mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Injinia Stephano Kaliwa akiongea na baadhi ya wananchi waliojitolea kufanya usafi eneo la Halmashauri ya wilaya ya Mlimba.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Injinia Stephano Kaliwa amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya wananchi kujitolea kufanya usafi katika eneo ambalo Halmashauri hiyo inategemea kujenga ofisi yake mpya.
Akizungumza katika eneo la tukio lambapo shughuli hizo zilkuwa zinaendelea, Injinia Kaliwa amewapongeza wananchi wa maeneo ya Mchombe kwa kujitolea huku akisisitiza kuwa kujitoa huku kwa wananchi kunaweza kupelekea baadhi ya gharama kupungua hivyo gharama zitakazobakia zitatumika katika kuboresha zaidi ofisi hiyo pamoja na shughuli nyingine za kiofisi ili kuhakikisha huduma kwa wananchi hao zinatolewa kwa utaratibu unaofaa.
Nae mzee Bakari amesema kuwa wamezoea kufanya shughuli hizi kutokana na ukweli kwamba wao ni miongoni mwa wananchi waliozoea kujitolea kwaajili ya manufaa ya wananchi na nchi kwa ujumla, kwa kuzingatia kuwa ofisi hiyo itawasaidia wao wenyewe katika kurahisisha upatikanaji wa huduma.
''Bila shaka tumezoea sana kujitolea kufanya shughuli hizi, tumezoea kujitolea kwa manufaa ya wananchi wetu na nchi kwa ujumla, hili ni kutokana na ukweli kwamba hii Ofisi itakapokamilika itatusaidia sisi wenyewe na jamii yetu kwa ujumla sasa kwanini tusijitoe?'' Alimaliza mzee bakari kwa namna ya kuuliza swali.
chini Habari picha zikionesha jitihada mbalimbali za wananchi kujitolea.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa