JSI Tanzania ni taasisi binafsi inayo jihusisha na utafiti wa Afya ya Jamii pamoja na uhusiano wa kijamii.Mkurugenzi wa JSI kanda ya Mashariki Mheshimiwa Shija Maganga alisema leo akiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kuwa JSI inafanya kazi za maendeleo ya Afya ya Jamii ikishirikiana na Serikali kupitia ngazi za Mikoa,Wilaya na Kata ikiwa na lengo la kusogeza hudumakwa Jamii hasa kumfikia mlengwa ambaye ni Watoto wanao ishi katika mazingira Magumu,watoto walio pata maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU) Pamoja na changamoto nyingine zinazo wakabili Watoto hasa wanapo fanyiwa vitendo kinyumena Maadili mfano vitendo vya ubakaji,hivyo JSI inashirikiana kwa karibu na serikali kupitia Afisa Ustawi wa Jamii kila Mkoana Kila Kata kusimamia kesi na mashauri ili kulinda haki za mtoto anaye ishi katika mazingira Magumu.JSI pia inatoa mafunzokwa wa wanajamii husika kwa lengo la kuwafikia walengwa kwa njia za ukusanyaji wa taarifa.
Mkurugenzi JSI kanda ya mashariki ameona kuna umuhimu mkubwa wa kuimarisha mifumo ya utoaji huduma kupitia watoa hudumakila Kata na vijiji kwa ujumla kwa kuwapatia msaada wa Baiskeli 10 pamoja na Kabati 11 za Kuifadhi taarifa muhimu za maendeleoya afya ya jamii mlengwa akiwa ni mtoto,akikabidhi msaada huo katika Halmashauri ya Wiliaya ya Kilombero.Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya yaKilombero Latifa Kalikawe ameipongeza JSI kwa kuwapatia Baiskeli pamoja na Kabati vifaa vitavyo tumika na watoa huduma ngazi za Kata na Vijijikuwafikia walengwa, huku Meneja wa Kizazi kipya Michael Mairinga akiwasisitiza watoa huduma kutumia msaada huo kwa lengo la kufikisha huduma kwa Jamii husika.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa