Pichani juu: Aliyesimama ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa, Pembeni yake ni mganga mkuu wa Halmashauri Dr. Christina Guveti
Kamati ya Afya ya msingi katika Halmashauri ya wilaya ya Mlimba mapema leo imekutana katika ukumbi uliopo kata ya mchombe kuweka mikakati kadhaa ya kuhakikisha kuwa wanatoa elimu ya kutosha ili wananchi waweze kuchanja Chanjo ya COVID 19 kwa hiyari
Akizungumza katika kikao hicho ambacho kimekusanya kada mbalimbali wakiwemo wauguzi, viongozi wa dini na watendaji kadhaa na wakuu wa idara, mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba ambae pia ndie aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho amesema kuwa tumekuwa na changamoto ya kupata mwitikio mdogo wa wananchi wanaokuja kuchanja kwa hiyari hivyo ni heri tukaweka mipango itakayosaidia kulifanya zoezi hili kuwa jepesi.
kwa upande wake kaimu afisa Chanjo Ndg Deo amesema kuwa mpaka sasa tumekwishapokea chanjo hizo 4000 ambapo katika kuhakikisha inakwisha, wilaya ilitenga vituo vitatu ambavyo ni Idete ambapo zimepelekwa chanjo 700, mngeta wamepata Chanjo 1700, Mlimba Chanjo 1450 pamoja na Utengule chanjo 150.
Aidha ndg Deo amesema kuwa mpaka sasa katika vituo vyote watu waliochanjwa ni 403 tu sawa na 15.6% ambapo wanawake ni 308 na wanaume ni 115 tu.
miongoni mwa mikakati ambayo kikao hicho iliamua ni kuwa kwanza, vituo vyote vinavyotoa huduma za Baba, Mama na mtoto viwe vinatoa elimu ya chanjo na kutoa chanjo hiyo kwa ujumla, pia kamati ihakikishe inaweka mipango ya kuhamasisha kwa Gari, pia vikao vya kamati ya Afya viwe vinafanyika mara kwa mara ili kuweza kubadilishana uzoefu na na taarifa za maendeleo ya chanjo, kutoa chanjo mkoba ni moja ya mikakati iliyoafikiwa pamoja na kuandaa elimu ya chanjo na kutoa chanjo sehemu zenye mikusanyiko.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa