Pichani ni mratibu wa UKIMWI Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Dkt Doroth Maganga.
Kwa masikitiko makubwa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero inapenda kukanusha vikali kuhusu kipande kidogo cha rekodi kinachosambaa kuwa Halmashauri haina dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV).
Hayo yamesemwa na Mratibu wa masuala ya UKIMWI wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Dkt Doroth Maganga, alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi mapema leo asubuhi ndani ya ofisi ya mganga mkuu wa Halmashauri hiyo.
Alisisitiza kuwa tayari wamekwisha mkamata binti huyo ambae anafanya kazi katika taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama SAUTI, na wameshamuhoji na amekiri kufanya hivyo na ameomba radhi kwa kitendo hicho kwani kwa mujibu wa maelezo yake alisema kuwa Dawa hizo zinapatikana katika Hospitali ya mtakatifu Fransis pekee na hivyo kuathiri wakazi wa maeneo ya mbali kama Mgeta Kidatu N.K Kipesa na kiumbali hivyo kuleta hali ya sintofahamu kwa wakaazi wa wilaya hiyo.
Aidha akijibu shutuma hizo Dkt Maganga alisema kuwa Hospitali hiyo ya mtakatifu Fransis imepata mradi wa majaribio ya dawa mpya ya kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI kwa watoto chini ya umri ya miaka mitano,ijulikanayo kama Loprinavili boosted with Ritonavir, ambapo wanahitajika jumla ya watoto 85 na mpaka leo tayari wamekwishasajiliwa watoto wapatao 63 tu na ni mradi unaotarajiwa kuisha mwezi wa nne mwaka huu 2018.
Hata hivyo ametakiwa kuhakikisha kuwa anarekodi kipande kingine cha sauti ambacho kinachokanusha kauli yake ya awali na kukirusha tena kwa njia ile ile ili kuweza kusawazisha makosa yake aliyoyafanya.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa