Katibu tawala mkoa wa Morogoro Mh. Clifford Tandari ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Kilombero baada ya kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2017.
Mh. Tandari ameyasema hayo katika kikao cha pamoja na wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa bonde la umwagiliaji mjini Ifakara tarehe 10.11.2017.
Katibu tawala huyo amewataka viongozi wa elimu, wadau wa elimu ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Kilombero kuendelea kuongeza juhudi walizozifanya kufikia hatua hiyo ya mafanikio ili kuendeleza ushindi huo kwa siku zijazo ikiwa ni pamoja na kufanya vizuri Zaidi ya hapo.
Halmashauri ya wilaya ya Kilombero katika matokeo ya Kumaliza elimu ya msingi 2017 yaliyotolewa na baraza la mtihani la taifa imeshika nafasi ya nne kimkoa kati ya Halmashauri tisa za mkoa wa Morogoro ambapo ufaulu huo ni sawa na aslimia 78.9 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo ufaulu ulikuwa ni aslimia 47 na halmashauri ilishika nafasi ya nane kimkoa.
Matokeo haya yamevunja rekodi ya miaka mitano mfululizo ambapo tokea mwaka 2012 rekodi hiyo haijawahi kufikiwa. Hata hivyo ufaulu huo umefikia malengo ya matarajio ya ufaulu halmashauri ya wilaya ya Kilombero iliyojiwekea.
Naye mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Mh. Dennis Londo alitumia nafasi hiyo kumweleza katibu tawala wa mkoa wa Morogoro mikakati ambayo halmashuri yake imejiwekea katika kukabiliana na upungufu wa vyumba 41 vya madarasa kwa shule za sekondari ambapo kwa sasa kila Kijiji kinaandaa benki ya matofali ikiwa ni matayarisho ya kuinua maboma ambayo mara yatakapokamilika halmashauri itayamalizia ili kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa vilivyopo sasa.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa