Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero Mh Dennis Londo katika kikao cha kazi cha watendaji wa kata na vijiji ambapo pia kiliwahusisha wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri.
Bwana Londo amewaeleza watendaji kuwa tatizo la mimba ni kubwa na hatuwezi kuendelea kuhubili maendeleo huku tukiwaacha watoto wetu wakiendelea kukumbwa na tatizo la ujauzito mashuleni, sababu inayopelekea tatizo hili kuwa kubwa ni utendaji mbovu wa watendaji wetu katika kuhakikisha wahusika wanakamatwa na wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Asilimia 90 ya kesi za ujauzito mashuleni zipo kwenye ngazi ya baraza la kata ambapo bado kesi hizo hazijapelekwa polisi, aidha Mkurugenzi mtendaji amewakumbusha watendaji wake kuhusu kutekeleza kile alichowaandikia ili kutekeleza jukumu la kuzipeleka kesi zinazohusiana na ujauzito kwenye vyombo vya sheria badala ya kuendelea kubaki nazo kwenye mabaraza ya kata. Amewataka watendaji kuepuka na tuhuma zinazowakabili kuhusiana na kupokea rushwa ili kuwalinda watuhumiwa wanaowapatia ujauzito wanafunzi.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa