Pichani juu: kutoka kulia Mohamed Ramadhani, Kaimu Mkurugenzi Kilombero, Robert Selasela, Katibu Tawala Kilombero, na Zakia Fandey, Kaimu Afisa Elimu msingi Kilombero.
Kilele cha juma la elimu ambacho maadhimisho yake yalifanyika katika shule ya msingi mkamba mwishoni mwa juma hili, yamefana sana huku yakiacha alama ya mafanikio makubwa sana kwa wazazi kwa kuibua upya ari ya wazazi kuchangia maendeleo ya shule zote za Kilombero hususan kwenye suala la chakula kwaajili ya watoto wao.
Akizungumza na wazazi na wadau wakubwa wa elimu waliohudhuria kwenye shughuli hiyo, mgeni rasmi ambae pia ni Katibu Tawala wa wilaya ndugu Robert Selasela amesema kupitia hotuba yake kuwa, itakuwa ni jambo la busara sana kwa wazazi kuweza kuchangia kwaajili ya watoto wao hasa kwa kipindi hiki ambacho wanafunzi wa darasa la saba wanajiandaa kwaajili ya mitihani yao ya mwisho.
Nae afisa elimu shule ya msingi, bi Zakia Fandey, kwa upande wake alisisitiza kuwa kwa sasa viwango vya elimu kwa kiasi Fulani kimepanda ingawa bado tunahitaji kuongeza juhudi kubwa kwa kuwasaidia watoto hawa kwa kuwachangia chakula kwa hiari wao wakiwa wazazi na wadau wa elimu kwa ujumla.
Aidha wanafunzi wa shule ya msingi kiswanya kutoka katika tarafa ya mang’ula katika wimbo wao wa kuhamasisha elimu bora katika kilele cha juma hili, walisisitiza kuwa ni bora kabisa kwa wazazi kuelewa vizuri sera ya elimu bure, kwani haimaanishi kutochangia maendeleo ya shule, hivy waliwashauri wazazi waweze kushirikiana na walimu ili waweze kufukia kwenye malengo wanayoyahitaji.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa