Pichani juu: waziri wa mifugo na uvuvi mh. Luhanga Mpina, akimkabidhi Afisa kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, Bw. Mohammed Ramadhani, kikombe kama zawadi ya jumla ya ushindi wa pili kwa mkoa wa Morogoro, kwenye maonyesho ya Kilimo ya Nanenane mapema leo.
Halmashauri ya wilaya ya Kilombero leo kwenye maadhimisho ya sikukuu ya wakulima ambayo kikanda yanafanyika Morogoro, wamefanikiwa kuchukua kikombe cha ushindi wa pili, kwenye ushindi wa jumla kimkoa kwa mkoa wa Morogoro baada ya kufanikiwa kuonyesha vitu ambavyo vimeleta mabadiliko makubwa sana kwenye Nyanja za ubunifu wa zana za kilimo na ufugaji.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero ndg Mohammed Ramadhani amesem kuwa ushindi huo si tu wa watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero bali ni wa wana Kilombero kwa ujumla, kwani wadau na wakulima pia wamefanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha kuwa tunafanikiwa.
‘’Kiukweli zawadi hii sio tu ya Watendaji wa Halmashauri tu, bali hata wadau wa kilimo katika halmashauri hii’’. Alisema.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mfugaji kutoka kilombero ndugu Sosoma Poneka, ameibuka kuwa mfugaji bora wa pekee kwa Kilombero.
Bwana Poneka amesema kuwa ushindi huo unatokana na ushauri bora anaoupata kutoka kwa watendaji wa Kilombero, lakini pia jitihada binafsi zimewezesha ushindi wake.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa