Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero ndugu David Ligazio amesema wataweka utaratibu wa kielimu kuwasaidia wanafunzi waliofeli waliokosa nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari wapate fursa ya elimu.
Haya amesema tarehe 29/1/2019 katika kikao cha baraza la kata la kupitia bajeti za kata kwa mwaka wa fedha mwaka 2019/2020 kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri wakati akijibu na kutolea ufafanuzi wa hoja mbalimbali za wajumbe.
Kikao hicho kilikuwa kikijadili masuala mbalimbali ndani ya bajeti pamoja na namna ya kuboresha bajeti hiyo,masuala la kupeleka fedha za madawati katika shule zote za sekondari ili yatimike na wanafunzi wanaojiunga na kidatu cha kwanza.
Aidha katika kikao hicho mwenyekiti Ligazio amewataka watendaji kata wakisaidiana na madiwani kujua taarifa za wanafunzi wasioripoti mashuleniā€¯watendaji wote kwakushirikiana na wadiwani hakikisheni mnapata taarifa za wanafunzi wote wasioripoti shuleni mwaka huu ili tujue matatizo yao pia kama hawataripoti nafasi zao tuwape wengineā€¯amesema Ligazio
Kikao hicho kiliongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wiliya ya Kilombero kilichowakutanisha wakuu wa idara mbalimbali,madiwani na watendaji wa kata.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa