Mratibu wa Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, ndg Nicholaus Makata, ameelezea hatua waliyofikia kwa hivi sasa juu ya tukio la mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, unaotarajiwa kupokelewa 5/8/2019 katika Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, kupitia eneo la kidatu kata ya Mkamba, ukitokea katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.
Ndg Makata amesema kuwa, kamati zote zimejipanga vizuri kuhakikisha shughuri zote za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, zinakwenda vizuri kama ilivyopangwa, na baadhi ya kamati hizo ni kamati ya ulinzi na usalama, fedha na mipango, chakula, hamasa na burudani, maradhi, usafiri, usafi na mazingira, pamoja na ujenzi.
Aidha Makata amesema kuwa, wataweza kutembelea miradi mitano, ukiwemo mradi wa maji uliopo katika kata ya sanje, elimu, kilimo, uvuvi na ufugaji bora wa samaki wa kisasa na utawala bora.
Hata hivyo, Mratibu huyo amesema kuwa, kwa upande wa kamati ya hamasa na burudani wameandaa wimbo mzuri kwa ajili ya Mwenge wa Uhuru, pamoja na vikundi mbalimbali vya kuburudisha katika eneo la miradi na mkesha, pia kwa asilimia kubwa ya waburudishaji wote wanatokea katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Sanjari na hayo Makata amewata wakazi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kujitokeza kwa wingi katika shughuri za kuupokea Mwenge wa Uhuru ili kuleta chachu na hamasa kwenye usherekeaji wa shughuri hiyo ya mapokezi ya Mwen ge wa Uhuru
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa