Pichani juu Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero, wabunge wa wilaya hiyo pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya jiji la Arusha wakiwa katika picha ya pamoja kwenye jengo la manispaa ya jiji la Arusha.
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya kilombero mwishoni mwa wiki hii walipata ziara ya kimafunzo kutembelea katika jiji la Arusha kwaajili ya mafunzo ya namna bora ya kuendesha mabaraza na kujifunza mambo mbalimbali ya maendeleo.
Madiwani hao wakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mhe. Daudi Ligazio walionekana ni watu waliojifunza mambo mengi na waliofurahishwa sana na safari hiyo, kwani kila walipoelekea kwenye vituo mbalimbali vya mafunzo walikuwa ni wenye kuuliza maswali mengi na kuchangia hoja nyingi ili kuweza kuambukiza maendeleo yaliyopatikana katika jiji hilo la Arusha katika halmashauri ya wilaya ya kilombero.
Aidha vituo ambavyo walipangiwa kutembelea madiwani hao ambavyo pia walivitembelea ni ukumbi wa baraza la madiwani, machinjio ya kisasa kabisa ya Arusha, sehemu ya kufugia nyoka ijulikanayo kama (Snake Park) na soko la kilombero linalopatikana katikati ya jiji hilo la Arusha ambavyo vivutio hivyo huchangia kwa kiasi kikubwa sana mapato ya jiji hilo ambayo hufikia wastani wa shilingi bilioni 13.
Akizungumza kwa niaba ya madiwani na wabunge waliotembelea eneo hilo, mwenyekiti Ligazio alisema kuwa wanashukuru sana kwa halmashauri kuwezesha safari hiyo ambayo pamoja na yote itasaidia kwa kiwango kikubwa suala la kuongeza mapato kwani kulikuwa na mianya mbalimbali ya upotevu wa pesa za serikali ambazo kwa namna moja ama nyingine wamepata njia za kuiziba na hivyo kuweza kuongeza mapato ya serikali.
Nae Afisa utumishi wa halmashauri hiyo Bwana Abdul Mbimbi, alisisitiza kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuisababishia halmashauri hasara kwa makusudi, kwani hakika hao watakuwa ni maadui wakubwa wa maendeleo ya halmashauri ya wilaya ya kilombero.
‘’Kwa sasa tunahitaji kuwa na halmashauri ya wilaya ya kilombero mpya kabisa kwani kwa kuangalia tu ni kwamba tunaweza na kutokana na mafunzo ambayo tumeyapata kwa wenzetu wa Arusha, tutahakikisha kuwa tunaboresha hali ya uchumi kwa kilombero na kuhakikisha kuwa uchumi unapanda kwa kubunivitega uchumi mbalimbali vikiwemo vile ambavyo manispaa ya jiji la Arusha wameshauri tuvifanye.’’ Alimaliza Ndg Mbimbi.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa