Pichani kutoka kushoto ni Afisa utumishi ndg Abdul Mbimbi, mgeni rasmi Mhe. Ndangalasi na Diwani wa kata ya Ziginali Ndg Shema Ndama, siku ya kufunga mafunzo hayo katika shule ya msingi ya Kiberege.
Mafunzo ya mabaraza ya kata yaliyokuwa yakiendelea kwa kata zote za halmashauri ya wilaya ya kilombero hatimae yamefungwa rasmi mwishoni mwa wiki hii katika kata ya ziginali.
Akifunga mafunzo hayo mwenyekiti msaidizi wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero Ndugu Ndangalasi alisema kuwa katika utekelezaji wa suala hili anahitaji kuona mabadiliko ya kiutendaji katika Ardhi na kama itatokea mabadiliko yoyote basi hakutakuwa na maana ya kuwepo kwa mafunzo hayo, aidha aliwasihi kuwa uwepo wao hapo ni katika kuzijua sheria za masuala ya ardhi na kwenda kuzitafsiri ili kuweza kuhakikisha wanapunguza baadhi ya migogoro ya ardhi kama sio kuimaliza kabisa.
Awali afisa utumishi wa wilaya ya kilombero bwana Abdul Mbimbi alisema kuwa mabaraza ya kata ni chombo muhimu sana katika kumaliza migogoro ya ardhi, awali kulikuwa na kesi nyingi sana zilizokuwa zinapelekwa Halmashauri, kabla ya mabaraza haya kujengewa uwezo, lakini kwa sasa anaamini kuwa, kuwepo kwa wajumbe hao ambao walijengewa uwezo kwa siku tatu kwa kila kata, kutasaidia sana kupunguza mzigo mkubwa wa kesi zinazohusiana na ardhi katika ofisi za Halmashauri.
Aidha diwani wa kata ya Ziginali ndugu Shema Ndama, aliwashukuru sana wawezeshaji ambao walitoka kwenye ofisi ya wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mgeni rasmi, ujumbe kutoka kwa mkurugenzi mkuu pamoja na wajumbe wote kutoka katika kata zote zilizokuwa za mwisho kwenye mafunzo hayo na kumuhakikishia mgeni rasmi kuwa, kwakuwa wajumbe hawa ni watumishi kama walivyo watumishi wengine, basi watafanya kazi na kuhakikisha kuwa kila jambo linakwenda kama lilivyopangwa na mwisho wa siku kesi zinazohusiana na masuala ya Ardhi zinapungua kama sio kuisha kabisa.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa