Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Eng. Stephano B. Kaliwa amesaini Mkataba wa Soma na Mti dhidi ya Afisa Elimu Sekondari Bi. Anibariki G. Ngata. Mkataba huo unahusisha juu ya Utunzaji wa Mazingira, upandaji wa miti pamoja na kuitunza miti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji ametaka kila mwanafunzi wa Sekondari awe na mti anaohudumia kila siku hadi atakapohimitu Elimu ya Sekondari.
Halmashauri ina jumla ya shule 32 na wanafunzi 16,523 ambao wanatakiwa kuihudumia miti hiyo na kuhakikisha inatunzwa na kupendezesha mazingira yote ya shule katika mihula yote ya masomo.
Mkataba huo ulikabidhiwa mbele ya Mwanasheria wa Halmashauri Wakili Kulaba G. Doto @dotogabriel pamoja na wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri @mazingirakwanzafoundation @mazingira_plus @mkonekti @kyobyad @dc.kilombero @mazingira @morogoro_ndio_home
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa