Halmashauri ya wilaya ya Kilombero imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Bilioni 1.66 kutoka katika vyanzo mbalimbali ya mapato na kuifanya Halmashauri kuvuka lengo la makadirio katika bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 kwa miezi sita kuanzia June mpaka Desemba ambapo imepanda kwa asilimia 9 nakufikia asilimia 59 toka 50 ya awali.
Aidha katika matumizi ya pato hilo Halmashauri imeanza kuwekeza na kutekeleza miradi mbalimbali wilayani humo ambapo katika ufafanuzi wa mikakati ya kimaendeleo kupitia kamati ya fedha tayari imetumia shilingi milioni 179 kwa kukopesha vikundi mbalimbali vya vijana na akina mama katika maeneo tofauti wilayani humo.
Hata hivyo mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero Chief James Ihunyo amesema vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo kwa awamu ya pili vimetoka na kuwataka madiwani na watendaji kata kutoa elimu ya kutosha kwa wafanyabiashara juu ya umuhimu wa vitambulisho hivyo.
“Vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo kwa awamu ya pili vimetoka viko ofisi ya mkuu wa mkoa tunakabidhiwa hivi karibuni ili kuwasaidia hawa wafanya biashara,naomba watendaji na madiwani tutoe elimu ya kutosha ili kila mfanyabiashara ajue umuhimu wa kuwa na kitambulisho kwa maana itafika wakati hataruhusiwa mfanyabiashara yeyote kuwa na biashara ndani ya halmashauri kama hana kitambulisho naomba fikisheni ujumbe huu”amesema Ihunyo
Ameyazungumza hayo katika kikao cha baraza la madiwani ambacho kimeongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Ndugu Daud Ligazio,kimehudhuliwa na Mkurugunzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero Eng.Stephano Kaliwa, maofisa utumishi kutoka idara mbalimbali, watendaji na wananchi wote wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero kwenye ukumbi wa mikutano tarehe 30/1/2019 ikiwa ni sehemu ya maboresho ya bajeti ya kwa mwaka wa fedha 2019/2020
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa