Pichani juu: Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero ndugu Faraja Nakua akionesha mfano wa kupandikiza mpunga katika hafla ya uzinduzi wa msimu wa kilimo katika wilaya hiyo.
Wakulima wilayani Kilombero wametakiwa kutililia mkazo uzalishaji wa mazao ya kimkakati ambayo ni Korosho,Chikichi pamba kokoa na miwa pamoja matumizi ya teknolojia bora za kilimo ili kumuunga mkono Rais wa jamhuri ya muungano waTanzania katika kuifikia Tanzania ya viwanda na kuifikia dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo imedhamiria kuifikisha Tanzania kwenye hadhi ya kipato cha kati na kuondokana na umaskini.
Wito huo umetolewa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero ndugu Faraja Nakua Desemba 20,mwaka huu katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa kilimo wa 2018/2019 iliyofanyika katika kijiji cha Njage wilayani humo uliokuwa na lengo la kutoa taarifa muhimu kwa wakulima ikiwemo kuwashauri wakulima kufanya maandalizi ya mashamba mapema.
Awali akizungumza katika uzinduzi huo wa msimu wa kilimo wilayani Kilombero, Afisa kilimo wa halmashauri hiyo Injinia Romanus Myeye alisema kuwa asilimia 80 ya wakazi wa wilaya hiyo wamekuwa wakitegemea kilimo kama shughuli kuu ya kiuchumi na kwa kulitambua hilo,halmashauri hiyo imejiwekea lengo la kulima hekta 181163 ambazo mazao ya chakula yatalimwa katika hekta 160161,biashara hekta 16823 na mazao mengineyo yakilimwa katika hekta 4180.
Pamoja na hayo Injinia Myeye amebainisha changamoto mbalimbali zinazoathiri shughuli za kilimo ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi,wadudu waharibifu kama vile viwavijeshi vamizi panya na upatikanaji wa npembejeo za kilimo kwa wakati huku akiwasisitiza wakulima kulima mazao yanayostahimili ukame.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Njage Bwana Mathew Chawala aliishukuru halmashauri ya wilaya ya Kilombero kwa kuboresha miundombinu ya kilimo ikiwa ni pamoja na uboreshwaji wa skimu ambayo mpaka sasa ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni 500 pamoja na ushirikiano wa wadau mbalimbali wa ppembejeo za kilimo pamoja na benki ya Dunia inayofadhili ujenzi wa skimu hiyo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa