Katibu tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Bw.Selasela amefungua mafunzo maaluma ya uimalishaji wa mfumo wa OPRAS(Open Perfomance Result Apraisal System) kwa wakuu wa shule za misingi na Sekondari wilayani wenye lengo la kuboresha ufanisi kazini
Mfumo huo wa OPRAS umejikita haswa katika kuwawezesha walimu kuweka malengo ya kiutendaji kwa kada ya ualimu unaotokana na maelekezo ya kazi ya mwalimu kama ilivyo ainishwa katika walaka kwa maendeleo ya utumishi Na.1 ya mwaka 2014 kuhusu miundo ya kiutumishi ya kada za walimu chini ya wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi sayansi na teknolojia
Akizungumzia katika katika uzinduzi huo leo tarehe 18/1/2019 katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari ya wasichana Ifakara,Selasela amewataka walimu wajifunze kwa umakini maarifa hayo kwa manufaa ya walengwa ambao ni walimu na baada ya mafunzo hayo, utekelezwaji uanze kwa kuwashirikisha walimu juu ya mfumo huu kuepesha malumbano ya majukumu ili kupata ufanisi wa kazi huku akiwaka wazi kusudi la serikali katika mfumo huo wa OPRAS kuwa ni muhususi kwa kuboresha taaluma nchini.
Aidha amewataka viongozi hao kuwa na nidhamu katika kutekereza majukumu yao na kuwahimuza watumishi walio chini yao ili kuleta maendeleo ya kielimu katika halmashauri “serikali haitasita kuwachukulia hatua walimu na viongozi wazembe ,niwaombe muwe na nidhamu katika uwajibikaji ili tulete maendeleo kwenye halmashauri yetu”amesema Bw.Selasela
Mafunzo hayo yameongozwa na afisa elimu msingi wilaya ya Kilombero Bi.Witness Kimoleta na maafisa wengine wa elimu ngazi ya wilaya,wathibiti ubora wa shule,ofisi ya tume ya utumishi wa walimu TSC na vingozi wa chama cha walimu Tanzania CWT wilaya.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa